Tahadhari Wasichana

Wasichana wengi siku hizi wanapenda maisha ya mteremko. Apate mtu ambaye ana gari, nyumba ya kisasa, accounts zilizojaa na anayempa kila anachohitaji. Sikatai kila mtu anapenda maisha mazuri, lakini fedha na uwezo wa mtu isiwe kigezo cha wewe kumkubali mtu akuoe. Fedha na mali ni vitu vinavyokuja na kutoweka, leo umekubali akuoe sababu ni mambo safi, zikiisha au akipunguzwa kazini utafanyaje?

Mali ni baraka za Mungu ambapo hata wewe ukifanya kazi kwa bidii na uaminifu utavipata. Hivyo usimwangalie mtu kwa kile alichonacho mfukoni, utu wa mtu haupo kwenye mali. Usipoteze furaha yako sababu mtu ambaye anakupa furaha ya kweli hana kitu hivyo unamuacha ilhali unajua kuwa ndio chaguo la moyo wako, unakimbilia kwa wenye mali. Ni afadhali kuishi katika maisha ya kawaida yenye amani na upendo wa kweli kuliko kuishi maisha ya kifahari yaliyojaa ugomvi na chuki.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s