Msaada wa Mungu katika Ujauzito

Shalom
Kwa wale wote wanaotegemea kujifungua, mwamini Bwana Yesu kuwa atakuvusha salama. Usikubali shetani akujaze hofu hadi ushindwe kuifurahia safari yako ya ujauzito. Mkabidhi Mungu kila hatua na mtumaini kuwa anakwenda kufanya. Mistari hii uikiri na kuitafakari kila siku, itakuondolea hofu na kukupa tumaini.

FLP. 4:6-7
“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

1 PET. 5:7
“huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”

ISA. 26:3-4
“Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.  Mtumainini BWANA siku zote Maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.”

ISA. 66:9
“Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.”

Advertisements

3 thoughts on “Msaada wa Mungu katika Ujauzito

  1. Naombeni mniombe kwani hapa tulipo mwenye nyumba wetu ana sadikika kua mchawi mimi siamini uchawi ila nakuwa na wakati mgumu pale unapo amka usiku na kumkuta akizunguka uwani anatutia hofu kwakeli.

  2. Du pole sana ndg yangu Alex. Hutakiwi kuogopa hasa kama umeokoka mchawi ni mtu mdogo sana. Ila kama bado hukaokoka ogopa sana na kimbia kwa Yesu utakuwa salama. Unatakiwa uombe na kukemea tu then ataogopa na hatarudia.

  3. Asante kututia moyo wajawazito maana kweli kuna changamoto nyingi ktk safari hii ya miezi 9. Ni baraka huu uumbaji wa Mungu!!!
    Amina kwa uhodari mkubwa, wamama wote juuuuuuuuuuuuuu!!!!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s