Mwanamke Kwenye Ndoa

Mwanamke, ili ndoa yako ilete mafanikio lazima utafute kwa bidii kuwa na sifa zifuatazo
1. Muombaji
Simama kama mlinzi kwa ajili ya familia yako. Maombi yataisimamisha ndoa yako na kuwavusha katika vipindi vigumu.

2. Mtii
Hii haina upinzani, biblia imemwagiza mwanamke kuwa mtii kwa mume wake katika Bwana. Usishindane na mume wako, mtii na pale anapokuwa mgumu kumtii maombi ndiyo silaha yako.

3. Mshauri
Wewe ni mshauri namba moja kwa mume wako hivyo tumia nafasi hiyo vizuri umshauri kwa busara na hekima na sio kwa kusukumwa na hasira, chuki, kukata tamaa au uchungu. Biblia inamifano ya wanawake walio washauri waume zao vibaya na matokeo yake yakawa majuto;  Sarah, hawa, mke wa ahabu na lingine mingi.

4. Mkarimu
Ukarimu kwa watu wote wanaokuzunguka bila kubagua au kuangalia wao wanakupa nini. Onyesha ukarimu kwa moyo uliochangamka. Nyumba inaonekana yenye ukarimu kwa kipimo cha ukarimu wa mke.

5. Msiri
Tunza siri za nyumbani kwako. Usipende kusema kila kinachotokea nyumbani kwako. Sio tu kila unapopishana kauli na mume wako unawaambia ndugu na marafiki zako au pale mume anapoyumba kiuchumi unawaambia watu. Hii sio sawa, mstahi mume wako kwa kutunza siri za ndoa yako.

6 thoughts on “Mwanamke Kwenye Ndoa

  1. Amina dada nimekupata. Mwanzon nilikua sijui ninaelekea wapi. Kwakusoma hapa mada mbalimbali kwakwel nimejiona ninamuhitaji Mungu zaid. Na haya ulotushirikisha nitaendelea kuyafanyia kazi. Asante sana kwa elimu unayoitoa na Mungu azid kukupa hekima na mwongozo wa nn cha kutuelimisha. Mungu akubarik.

  2. Bwana Yesu asifiwe. Mungu akubariki sana kwa mafundisho yako ambayo naweza kusema ni mazito na yana ujumbe wenye kutia moyo sana. Mimi nilikuwa naomba ushauri, nimeolewa na nina mtoto mmoja; nimeokoka na nampenda Yesu. Tatizo ni huyu mwenzangu, nimejitahidi kutafuta mitaji afanye chochote kuinua kipato cha familia lakini matokeo yake anafuja tu pesa bila kufanya chochote cha maana. Alikopa benki katumia anavyojua na sasa yupo tu. Nahofu kutafuta mtaji nimpe kwani haonekani kama mtu wa kazi. Kwa sasa ni mjamzito, nafanya kazi na majukumu ya nyumbani ambayo angeweza kusaidia ila sielewi kama ni kiburi au uvivu maana hakuna anachofanya zaidi ya kulala mpaka atakapopenda kuamka na kwenda zake kuzurura. Je, ni kweli huu ndio wajibu wa mume? Nishauri dada yangu maana niko dilema na nimekata tamaa sana ya maisha ya ndoa. Mungu akubariki.

  3. Bwana Yesu asifiwe. Mungu akubariki sana kwa mafundisho yako ambayo naweza kusema ni mazito na yana ujumbe wenye kutia moyo sana. Mimi nilikuwa naomba ushauri, nimeolewa na nina mtoto mmoja; nimeokoka na nampenda Yesu. Tatizo ni huyu mwenzangu, nimejitahidi kutafuta mitaji afanye chochote kuinua kipato cha familia lakini matokeo yake anafuja tu pesa bila kufanya chochote cha maana. Alikopa benki katumia anavyojua na sasa yupo tu. Nahofu kutafuta mtaji nimpe kwani haonekani kama mtu wa kazi. Kwa sasa ni mjamzito, nafanya kazi na majukumu ya nyumbani ambayo angeweza kusaidia ila sielewi kama ni kiburi au uvivu maana hakuna anachofanya zaidi ya kulala mpaka atakapopenda kuamka na kwenda zake kuzurura. Je, ni kweli huu ndio wajibu wa mume? Nishauri dada yangu maana niko dilema na nimekata tamaa sana ya maisha ya ndoa. Mungu akubariki sana.

  4. Asante kwa mafundisho yako mazuri. Maombi ndiyo silaha ya ndoa.
    Mungu awabariki sana. Mama Anny Mushi

  5. Wamama tusiache kumlilia mungu kwa hakika ndoa zetu zitapona na tutamshukuru mungu kwa mambo makuu ambayo tulifikiri hayawezekani kumbe yanawezekana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s