Mchumba Siyo Mume!

Umeokoka na unamtumikia Mungu. Una mchumba naye ameokoka na anamtumikia Mungu. Tambueni kuwa shetani hajalala usingizi na miili huwa haiokoki bali roho na hatuenendi kuufuata mwili bali roho. Mnapokuwa kila wakati mnaongelea na kuchat about sex ni rahisi sana kujikuta mnaufuata mwili badala ya roho. Unapokuwa mchumba haujawa mke hivyo angalia sana unapoanza kufanya majukumu ya mke unaweza kujikuta umeshamkosea Mungu.

Hamjaona lakini unaufunguo wa nyumba/ chumba cha mchumba wako, unamfulia, kumtandikia kitanda, kumpikia, kumwandalia maji ya kuoga na unakaa kwake hadi saa sita za usiku wawili tu. Mnajipa moyo hamjamtenda Mungu dhambi maana hamjazini lakini mefanya mengine yote hadi kufikia kuamshana hisia za viungo vya uzazi. Je unaujasiri mbele za Mungu kwa hayo unayoyafanya? Dhamiri yako haikushuhudii kuwa unaenda njia siyo? Kama umeweza kusubiri miaka yote kwanini ushindwe sasa ambapo na mipango ya kuoana mmeshapanga?  

Naongea na wewe binti unayesema umeokoka na Yesu ni Bwana, kama umeamua kuokoka basi amua kikamilifu. Msiifuatishe namna ya dunia hii, onyesha msimamo kama kwa Mungu au kwa shetani. Purity starts from the heart, thoughts, words then actions. Siwezi kukupamba kwa maneno mazuri wakati najua unakosea na kuelekea kuangamia. Mchumba sio mume, acha kufanya majukumu ya mke kabla hujawa mke.

Advertisements

One thought on “Mchumba Siyo Mume!

  1. Asante kwa mada hio, mchumba si mke.
    Hapa ndipo vijana wengi tuna mkosea Mungu na kujidayi tumeokoka.
    Uhauri wangu kwa wachumba ni huu: Hepukeni kuongelea sehemu inayo Hepukeni kuongelea sehemu inayo jificha.
    Hepukeni maongezi inayo leta nyege. Mda wowote atakaye kuambia mfanye tendo la ndoa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s