Mungu Hufufua Ndoa Iliyokufa

Alikuja kama kijana mpole, mtanashati, mwenye upendo wa kweli, anayejali na mcheshi. Akakuonyesha mapenzi ya kweli, akakujali na kukuthamini. Haukuona jambo lolote baya kwake, haukuona sababu ya kumkataa. Ukamkubali, mkaoana kwa chereko na vifijo.

Sasa hata mwaka haujaisha kwenye ndoa amebadilika, sio yule kijana mpole na anayejali tena. Amekuwa mkali, asiyekusikiliza, hajali hisia zako, hana muda wa kukaa na wewe, controlling na anayekosoa kila umachofanya. Huna tena furaha kwenye ndoa yako na huwezi kumweleza mtu maana kwa watu anaonekana mstaarabu na mcheshi. Unaumia moyoni, unatamani kuondoka lakini huwezi, mto wako umejaa machozi maana unalia mwenyewe usiku. Watu wa nje wakikuona wanatamani ndoa yako maana hawajui maumivu yako.

Usiendelee kulia mwenyewe, lipo tumaini. Bwana Yesu anaweza kuweka uhai kwenye mifupa mikavu. Ndoa yako imekuwa kama mifupa mikavu, mwite Yesu awezaye kuifufua na kuihuisha tena. Samehe, uchungu utakuzuia kuomba na kupokea. Msamehe na mtendee wema hata kama hastahili hata kidogo, haufanyi kwake bali kwa Bwana. Mweleze Mungu maumivu yako na yeye pekee ndiye msaada wako. Usimchukie mumeo maana ndio wako wa maisha, mpende, muombee na msamehe. Bwana Yesu akuwezeshe na kukutia nguvu, jua hauko peke yako bali Mungu yupo nawe. Nakuombea.

Advertisements

2 thoughts on “Mungu Hufufua Ndoa Iliyokufa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s