Kwanini Unakataa Mtoto?

Leo nije kwa wakina kaka. Kwakweli sikufahamu kuwa hadi miaka ya dot com bado watu wanakataa ujauzito na watoto, really???. Wakati unafanya tendo hilo na huyo dada hukujua matokeo yanaweza kuwa nini? Wako wapi vijana wanaojua thamani ya msichana na kumsubiri hadi siku ya harusi? Wako wapi vijana wanaosimamia na kuamini wanayoyasema? Vijana wa siku hizi wamejaa mashairi mazuri mno ya mapenzi, yani maneno yao yanawamaliza kabisa wadada hata wakilokole wanajikuta wametoa yote. Inapotokea mimba basi huruka mita mia, kama sio yeye kabisa, mashairi ya kubembeleza yanageuka mikuki ya kuchoma moyo!

Umeshamkosea Mungu, dada amepata mimba ni jukumu lako kuutambua ujauzito huo na kuulea pamoja na mtoto. Wengine wanawashauri wasichana watoe mimba na wasichana kwa kutokujua la kufanya wanakubali. Ni jambo la aibu sana kukataa mimba na mtoto wako, na akishafika miaka mitano unajitutumua mahakamani kumdai mtoto, mbaya sana.

Wewe kijana unayesoma hapa, Mungu anajua ni watoto wangapi umewakataa, Tubu sasa mbele za Mungu na haraka uende ukaombe radhi kwa mama watoto wako na ukubali majukumu yako.

Advertisements

3 thoughts on “Kwanini Unakataa Mtoto?

  1. Naomba uandike na kuhusu maumivu wadada wapendwa wanayotuachia wakaka kwa kutushawishi hadi kuanguka kwenye uzinz kabla ya ndoa…maana sijui kama unafahamu nyakati hizi wadada wanaongoza kutushawishi hadi unakuta mtu unaanguka kwenye ngono wakiamini kuwa akipata mimba utamuoa…ushawishi wao na maneno yao laini ni wa hatari sana..naomba ufanye utafiti na uje uandike humu!

    Ni vile vijana wa kiume hatuongei kwa kulalamika lakin hali ni mbaya sana..ukionyesha msimamo wa kutotaka ngono kabla ya ndoa utashawishiwa weee hadi kuvumishiwa kuwa labda wewe ni gay…sijui ni wapi tuelekeze malalamiko yetu!

  2. Mungu awasaidie kwa kweli, wajue wajibu wao, na nini wafanye kwa wakati ulio sahihi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s