Tenda Mema Kwa Watu Wote

GAL. 6:10
“Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”

Ni agizo tumepewa kadiri tupatapo nafasi tuwatendee watu mema. Unaweza kuwatendea watu mema kwa sababu ya upendo ulionao kwao. Inapotokea mtu huyo akakukosea ni ngumu sana kumtendea mema, au mtu ambaye haonyeshi shukurani. Ndipo inapokuja sababu ya pili ya kuwatendea watu wema: upendo wako kwa Yesu. Bwana alimwambia petro kama unanipenda lisha kondoo wangu, chunga kondoo wangu. Upendo wetu kwa Yesu unatufanya tuwatendee watu mema hata kama kibinadamu ni ngumu. Lakini mara ngapi upendo wetu kwa Yesu umeyumba kutokana na mambo tunayokutana nayo?

Sababu pekee ambayo haibadiliki na ya kuaminika ya kukufanya kumtendea mtu mema hata kama hastahili kabisa ni upendo wa Yesu kwetu. Huu ni upendo usiobadilika, upendo usio na kikomo, upendo wa agape. Tazama upendo wa Yesu kwako anavyokutendea mema usiyostahili nawe uwatendee watu wote mema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s