Ikimbie Zinaa

1 KOR. 6:18-19
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

Wako wapi vijana wanaomheshimu Mungu? Vijana wanaofahamu kuwa miili yao ni hekalu la Roho mtakatifu. Vijana wanaoishi maisha matakatifu wakiwa nyumbani, kazini, chuo, kanisani au michezoni, iwe mchana au usiku wao siku zote wanamtukuza Bwana kwa kinywa, moyo na miili yao? Vijana ambao hawakumbwi na wimbi la utandawazi na kumkosea Mungu? Vijana ambao hawabishani kuwa wapi kwenye biblia wameandika usimpe busu la ulimi mchumba wako, na wapi pameandikwa usimshike shike mchumba wako?

Vijana waliotayari kuikimbia zinaa hata kama watatengwa na rafiki zao. Wapo tayari kulishika neno la ushuhuda wao hata kama wataonekana hawapo kamili. Vijana wanaoijua kweli ya neno la Mungu nayo kweli imewaweka huru, sio huru kutenda dhambi bali huru mbali na dhambi. Mungu anatafuta waabuduo halisi wamuabudu katika roho na kweli, sio roho tu bali na kweli ambayo katika Yohana 17:17 biblia inasema hiyo kweli ni neno la Mungu.

Kuokoka sio fasheni, sio kuimba na kucheza madhabahuni, ni kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha na kumkataa shetani na mambo yake yote.

Advertisements

4 thoughts on “Ikimbie Zinaa

  1. ha ha kwa kweli nimecheka sana niliposoma hii topic hasa kwenye busu la ulimi…uliyosema ni kweli kabisa ndio yanayotokea siku hz kwa vijana wapendwa….lakini Magreth labda tutafakarishe ni nini chanzo cha haya?

    Me nadhani viongoz wa kanisa hasa ya walokole hawasimami ipasavyo kukemea dhambi…siku hz injili inahubiriwa mambo machache kama mafanikio bila kugusa dhambi ndio maana ndoa nyingi zinafungwa zikiwa na mimba tayari. Pia tunajua Mungu wetu ni wa rehema sana na ndio kinachofundishwa zaidi na kufanya baadhi ya vijana kuona kuwa hata wakianguka rehema itawasaidia (which is true).

    Pia ingefaa kila kwenye ibada itengwe angalau dakika tano-kumi tu kukemea hii dhambi ya uzinzi kwa sisi vijana..nimepata uzoefu katika hili hasa pale napohudhuria ibada/semina/kusoma makala zinazokemea uzinzi wa aina zote mara nyingi nikitoka hapo huwa na hofu sana na Mungu na kwa kwel siwez rudia hadi muda upite sana..so kama hili suala lingekuwa linasisitizwa kila palipo ibada hakika vijana tusingemkosea Mungu. Ni vile tu viongozi wa kanisa wanasahau kusisitiza lakini kibiblia uzinzi ni kitu kibaya sana kwa Bwana na kama ni vijana ujue kabisa taifa lijalo ndio linaharibika kabisa

    Dan

  2. Dah moyo uu radhi lakin mwili unakua dhaifu ee mungu niwezeshe kuyapenda ya rohoni na sio mwilini.na mwisho wa uasheati ni fedhea

  3. najengwa na hili, cha msingi tukaa katika neno. Neno likisema tukimbie basi tukimbie kweli na sio kukemea kwani waweza kuwa katika kibano cha mtego ukakemea huku unavuliwa nguo, na mwisho ukajikuta umesha anguka huku unakemea, “KIMBIA ZINAA”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s