Kuepukana na Tamaa ya Uasherati na Uzinzi

Watu wengi wanalalamika wanampenda Mungu lakini wanashindwa kujizuia na uasherati na uzinzi. Sasa tufuatilie somo hili, ni refu kidogo ila litakusaidia.

1 THE. 4:3-5, 7-8
“Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.”

Ni agizo la Mungu kila anayesema anamfuata Yesu aishi maisha matakatifu. Kushiriki tendo la ndoa na mtu ambaye si mke/mume wako ni dhambi, hii ni kwa wenye ndoa au wasio na ndoa. Miili hujaribu na wengi wamejaribiwa, ila kama umeokoka na umejazwa Roho mtakatifu unauwezo wa kushinda jaribu. Ni lazima uutawale mwili wako na mawazo yako.
MT. 5:28
“lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”

Biblia imasema kila mmoja hujaribiwa kwa tamaa yake, pale unapokuwa unatamaa ya kitu fulani ndipo na jaribu linapokuja. Hapa ni lazima kuhakikisha mawazo yako Mi safi. Usiruhusu mawazo yasiyofaa yapate nafasi ya kustawi na kujengwa ndani yako, maana yatapelekea kutenda dhambi. Hatuishi kwa kuifuatisha miili yetu bali roho ambazo zimekombolewa na damu ya Yesu. Unaporuhusu tamaa ichukue mimba itazaa dhambi na dhambi ikiwa ndani ya moyo wako itakupelekea kutenda yale ambayo unajua kabisa ni dhambi ila unashindwa kujizuia kutenda.

RUM. 7:17-20
“Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.”

Unapoufuata mwili utayafikiria mambo ya mwili na kufuata matakwa ya mwili. Lakini moyo wako ukijawa na Roho mtakatifu, hautafuata tamaa za mwili bali utautiisha mwili ufuate roho.

RUM. 8:5-10
“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.”

GAL. 5:16-17
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.”

Hili ni jambo la kujikana na kukubeba msalaba wako mwenyewe. Sio jambo la kusubiri mchungaji akukumbushe au hadi mahubiri ya kutisha, kama umeamua kumfuata Yesu basi usiishi kuufuatisha mwili. Omba kwa bidii na kutafuta kumjua Mungu na neno lake. Uwe na muda wako wa kuomba na kusoma neno la Mungu kila siku. Roho yako ikilishwa itakuwa na nguvu ya kushindana na mwili. Hii ni vita na ni lazima upigane vita vizuri na upate ushindi. Usiifuatishe namna ua dunia hii bali ufanywe upya katika kristo na kuitoa mwili wako kuwa dhabihu takatifu ya kumpendeza Mungu.

Advertisements

10 thoughts on “Kuepukana na Tamaa ya Uasherati na Uzinzi

  1. bwana yesu asifiwe,somo limenigusa sana mana na limenitia nguvu mana nami ninatatizo kama hilo.

  2. Ubarikiwe mtumish masomo kama haya yanafaa kwa vijana maana yanawasaidia wale wenye kushidwa kuuweza mwili nimevutiwa na somo hili stay blessed

  3. NICE TEACHING MAY ALMIGHTY GOD HELP ME TO WIN THIS BATTLE THAT I MAY GLORIFY HIM IN EVERLASTING

  4. AMEN,KWANZIA SASA NATAMKA KUUSHINDA MWILI NA TAMAA ZAKE ZOTE KATIKA JINA LA YESU KRISTO.AMEN

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s