Muangalie Mungu na Sio Wanaokuudhi

Huwezi kuwazuia watu kukunenea mabaya, wala kukuwazia mabaya. Unaweza kutenda mema na kujitoa kwa kila mtu lakini ukaishia kusagiwa meno na kupigwa mawe. Utakavyojibu na kutenda baada ya kufanyiwa mabaya unauwezo wa kuamua na kuzuia. Ukiangalia maneno na mawe wanayokurushia huwezi kumuona Mungu katika hali hiyo unayopitia zaidi utawaona watu walivyo wabaya na kuwawazia kisasi.

Stephano aliposagiwa meno hakuwaangalia wanadamu bali aliinua macho mbinguni na akauona utukufu wa Mungu. Unapokaza macho yako mbinguni na kuuona utukufu wa Mungu hautakuwa na kisasi juu ya wanaokutendea mabaya na kukupiga mawe bali upendo na msamaha juu yao. Usiangalie wanaokurushia mawe, kaza macho mbinguni uuone utukufu wa Mungu.

MDO 7:54-56, 60a
“Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s