Ee Mungu Nisaidie…

Kwa wewe uliyeonewa, sali sala hii mbele za Bwana …

ZAB. 69:1-5, 8, 12-20
“Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.
Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka.
Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu.    Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu.
Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. 

Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu.    Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,
Na msikwao kwa wana wa mama yangu. 
Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.   
Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao;

Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.  Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama.
Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji.  Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu. 

Ee BWANA, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.  Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.  Uikaribie nafsi yangu, uikomboe, Kwa sababu ya adui zangu unifidie.   
Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. 

Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.”

3 thoughts on “Ee Mungu Nisaidie…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s