Mume Kumpenda Mke

EFE. 5:25, 28-29
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa”

Mume kumpenda mke ni agizo. Agizo hili halibadiliki mke akiwa mkorofi, sio mtii au vyovyote vile. Biblia inamuagiza mume ampende mke kama kristo alivyolipenda kanisa. Huu ni upendo mkubwa sana, japokuwa kanisa lilikengeuka mbali naye bado upendo wa Kristo haukubadilika. Kumpenda mwanamke kama mwili wako mwenyewe, kumjali na kumtunza.

Ni rahisi sana kwa mwanamke kuonyesha utii pale anapoonyeshwa upendo. Wanaume wengi huonyesha upendo wakiwa wanachumbia ila wakishaoa tu wanajisahau na kusahau kama mke anahitaji upendo ili aweze kutimiliza majukumu yake kama mke vizuri kwa furaha. Upendo unaanzia kumjali hisia zake, kumtunza kimahitaji na kumtia moyo, kumsifia na kumuonyesha unamthamini.

Mwanamke anahitaji kujua unampenda kwa wewe kumweleza hivyo kuwa unampenda na kumtendea matendo ya upendo. Wanawake wengi hukosa hamu ya faragha na waume zao kwasababu huona kama wanapendwa kwa ajili hiyo tu. Mume siku nzima anamkaripia mkewe, hamsikilizi wala kumjali na usiku anaonyesha kuwa anamhitaji saana, huo sio upendo ambao mke anahitaji toka kwa mume wake.

Mume anapoonyesha kumsikikiza na kujali ushauri wa mkewe na kushauriana naye kabla hajafanya jambo lolote mke anaona anapendwa sana na yeye atazidisha upendo na heshima kwa mumewe. Mpende mkeo ili aweze kukuheshimu kwa furaha na sio kwa kujilazimisha. Kumpenda mke ni kujipenda mwenyewe. Mara moja moja mtoe out bila watoto na umueleze unavyompenda, zawadi sio lazima siku ya sherehe au kitu kikubwa, hata chocolate(unanunua kwa ajili yake na sio watoto), mke atahisi kupendwa sana.

Advertisements

2 thoughts on “Mume Kumpenda Mke

  1. Namshukuru mungu kwakupata kusoma neno hili na kupata aman ndan ya moyo wangu.naomba kama itawezekana hata mnitumie mafundisho mengne kwenye imel yangu.mim mume wangu aliokoka ila nimzinifu,kanitelekeza na watoto wawili,sina kazi.alininyanyasa sana,nikamfumania na huyomwanamke aliyekuwa ananisumbua kipndi nnamimba ya mwangu wapili.naomben sana maombi yenu ili mumewangu arudi tulee watoto.kwan ametekwa na huyo kahaba,hajari familia.mwanamke mwenyewe amemtorosha bila hidhin ya wazaz wake huyo mwanamke.

  2. Nimependa sana mafundisho hayo. Wanaume tuwajibike kwa wake zetu na tujitoe kwa familia zetu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s