Baraka za Rohoni

EFE. 1:3-4
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.”

Watu wengi huhangaika huku na huko kutafuta baraka za mwilini lakini hawafanyi lolote kutafuta baraka za rohoni. Mungu huwapa watoto wake baraka za mwilini na za rohoni pia. Msingi wa baraka za mwilini ni kujaa baraka za rohoni. Shetani hupambana jitihada zetu za kutafuta mafanikio hivyo unapokuwa na baraka za rohoni unakuwa na uwezo wa kumshinda shetani.

Kadiri roho zetu zinavyofanikiwa ndivyo na maisha ya mwilini yatafanikiwa. Baraka za mwilini bila ya za rohoni hazitakuwezesha kumshinda shetani. Vitu vya mwilini ni vya muda mfupi ila vya rohoni vinatupelekea uzima wa milele. Usitumie maisha yako yote kutafuta vya mwilini ukasahau vya rohoni maana utaishia kwenye hasara ya milele.

2 KOR. 4:16-18
“Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s