Shughulika na Maisha Yako

Yusufu aliuzwa na ndugu zake, baadaye alifungwa kwa kusingiziwa. Hayo yote hayakumzuia kufanya kazi kwa bidii na kufikia ndoto zake. Hakuwaweka ndugu zake moyoni wala kuwa na kinyongo nao. Alipopata madaraka aliwasaidia na kuwatunza na hatusomi kuwa alinlipiza kisasi mke wa potifa. Hali yake ya kuwa mfungwa haikumzuia kuja kutawala.

Maisha yako ya nyuma hayana nafasi katika maisha yako ya sasa na yajayo. Kwamba umeishi kwa kuteseka sana, umenyanyasika, umesimangwa basi wewe uwe mnyonge na wa kusaidiwa tu, hapana. Maadamu upo hai unanafasi ya kuboresha maisha yako. Huwezi kubaki unalaumu wazazi hawajakupeleka shule, mama wa kambo kwa kukutesa, mwalimu kwa kukufelisha, ndugu kwa kukutenga n.k na kuacha kutumia fursa uliyonayo hata kama ni ndogo kuboresha maisha yako. Kila mtu amepitia na anapitia matatizo lakini hayatufanyi kulaumu wengine na kukosa furaha.

Unapomwamini Mungu kuwa yupo upande wako daima utakuwa mwenye furaha, kuchangamka na mwenye matumaini. Mungu anaweza kukuinulia watu wa kukusaidia, na watu hao hawalazimiki kukusaidia hivyo chochote unachofanyiwa na mtu kipokee kwa moyo wa shukrani na kuzidi kumwangalia Mungu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s