Msichoke Kutenda Mema..

GAL. 6:9-10
“Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”

Hii mistari tumeizoea na inaonekana myepesi sana lakini linapokutokea la kukuvunja moyo kweli inahitaji neema ya Mungu kuitimiza. Nimekuwa nikiwapa maneno ya kuwatia moyo kila siku, nami pia ni mwanadamu leo nahitaji mnitie moyo ndugu wapendwa. Please sema neno la Mungu kwa ajili yangu na Mungu akubariki.

Advertisements

7 thoughts on “Msichoke Kutenda Mema..

 1. Mimi ni msomaji wa muda mrefu na hubarikiwa sana na blog hii ila sikuwahi kutoa comments hata siku moja. Leo Bwana amenipa neno hili kwa ajili yako:

  Mpendwa wangu,Paulo alisema 1Kor9:27b “isiwe nikiisha kuwahubiri wengine,mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
  Pamoja na dhiki,taabu,raha,utajiri etc vya huku duniani,nakuombea ndugu yangu siku ile ya mwisho uwe mmoja kati ya wale watakaomlaki Yesu mawinguni.

  Mungu aliyekupa kufanya kazi yake kwa njia hii akupake mafuta na kukuwezesha zaidi,taabu yako siyo bure katika Bwana.
  1Kor15:58 “Basi,ndugu zangu wapendwa,mwimarike,msitikisike,mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote,kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana ”
  Nakuombea uendelee mbele!

 2. Shalom!

  Namshukuru Mungu wetu wa upendo kwa afya na uzima atupao siku hadi siku. Hakika ni kwa neema zake tupo mpaka leo.

  Ninafurahi sana kuwa mmoja kati ya wengi ambao wanabarikiwa na kujengwa kupitia blog hii. Nakupongeza sana kwa kazi nzuri. Kuna roho nyingi sana unaokoa na maisha ya wengi unayajenga kwa kupitia mafundisho haya.
  Neno la Mungu linasema katika Luka 15:10, ‘Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.’ Ni wazi kuwa wewe unayeingiza watu katika ufalme wa Mungu na kuwaleta kwake Mungu wetu anakuona na hakika baraka zake zi juu yako na katika yote unayofanya. Changamoto lazima ni nyingi katika utume lakini thawabu yake ni kubwa.
  Songa mbele na Mungu akubariki sana.

  Amani ya Kristu Yesu izidi kuwa nawe siku zote za maisha yako.

 3. MUNGU wangu ninayemwamini, yuko pamoja na wewe.
  no matter what you are going through focus on HIM ,najua inawezekana si rahisi but put your trust in HIM.
  uweze kuziona distraction na obstacles kwa jicho la Rohoni na ukumbuke chochote kilichozaliwa na Mungu kimeushinda ulimwengu.
  Tunakuombea

 4. Mungu akubariki sana uzidi kutufundisha zaidi ya haya,kweli nabarikiwa ninaposoma kwan nipo kwenye wakati mgumu sana,naitaji kutiwa moyo na mniombee msiniache peke yangu ktk wakat mgumu namna hiyo

 5. Bwana Yesu asifiwe! kazi ya Mungu uifanyayo ina thamani kubwa sana machoni pa Mungu.Najua wewe ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine ambaye lazima apitie majaribu hasa baada ya kumkiri Yesu kama Bwana na mwokozi wake.Na shetani yupo tu akizungukazunguka kutaka kukumeza,Nakutia moyo songa mbele huku ukimtazama yeye aliyeianzisha kazi hiyo,atakushindia, anaithamini kazi yako.
  Mimi binafsi naamini Roho mtakatifu amekuwa akisema na mimi kupitia blog hii kwa sababu huwa napitia mapito na kimbilio langu huwa ni ktk blog hii kabla sijaanza kuomba .Mfano siku za nyuma ulizungumzia kusamehe. Yaani lile Neno lilikuwa langu kabisaaaa. na kupitia Neno hilo nilipona Roho. Mungu akubariki sana na uonapo unakosa mwelekeo mwambie wewe uliyeanzisha kazi hii utanifanyia njia. Tuko pamoja mtumishi wa Mungu, nakuombea pia

 6. Asanteni sana wapendwa. Mmefanyika baraka na faraja sana kwangu. Mungu azidi kuwabariki na kuwainua.

 7. Mungu akubariki sn sana kwa maneno mazito , kweli yananijenga sn nakunipa nguvu yakuendelea bila kukata tamaa. Ubarikiwe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s