Jambo Gani La Upendo Umetendewa Hutalisahau?

Mambo madogo ya upendo ambayo tunawafanyia watu au watu wanatufanyia hukaa daima ndani ya mioyo yetu. Mara nyingi huja wakati kunauhitaji mkubwa na mtoaji anaweza asielewe. Taja jambo moja ambalo mtu alikufanyia na kwako limekuwa ni kubwa na utamshukuru siku zote na huwezi kusahau wema huo.

Nianze: Rafiki wa mama yangu alipojitolea kuwa nami hospitali nilipokuwa nimelazwa, kunihudumia na hadi kufua nguo zangu wakati familia yangu yote ipo mbali nami. Kweli sitasahau jambo hili.
Karibu na wewe…

Advertisements

4 thoughts on “Jambo Gani La Upendo Umetendewa Hutalisahau?

 1. Ubarikiwe sana dada,. kiukweli unatufundisha sana kwa sisi tunaosoma neno la Mungu mara kwa mara. Nimependa sana post zako japo mimi sio mwepesi wa kucomment ila ninatafakari na ninakuombea kwa Mungu usichoke kumhubiri Mungu kwa njia ya mtandao. Bwana Yesu Asifiwe sana. Murwa Clara.

  ________________________________

 2. Dada yangu alipoamua kuacha mambo yake binafsi na kuhakikisha ananisomesha mimi kwanza, nilipofika mahali pa kujiweza mwenyewe ndio akaanza kujishugulisha na maendeleo yake. Siwezi hata siku moja kusahau

  Angelina Stephen
  Compassion International Tanzania
  Partnership Training and support Manager
  P.O.Box 3064
  Arusha
  Email:astephen@tz.ci.org
  Email:myangelika2000@yahoo.com
  Skype:angelstephen11

  “Not by Power nor by Might…”

 3. Shalom!
  Hakika sitasahau marafiki zangu wanne ambao nilikuwa nasoma nao chuoni. Nikiwa nimebakisha siku mbili kufanya mtihani wa kumaliza chuo, baba yangu mzazi alifariki. Nilitamani kuahirisha mitihani kwani hata maandalizi yalikuwa hayajakamilika. Wao waliungana na kunipa moyo na kunisaidia kusoma maeneo muhimu nifanye mtihani. Upendo wao wa kutumia muda wao kunifariji na kunisaidia hali si ndugu zangu ni kitu ambacho daima sitasahau, japo ndani ya chumba cha mtihani nilikaa peke yangu. Mungu azidi kuwabariki sana na daima nawatakia mema.

 4. ni upendo mkubwa alionifanyia mume
  wangu.amenisomesha kuanzia fomu one mpaka chuo kikuu.sitasahau upendo huu.maana kanitoa mbali.namshukuru mungu sana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s