Hujaolewa Umri Unaenda: Usikate Tamaa

Unamiaka zaidi ya 35, hujaolewa na wala huna mchumba. Rafiki zako wote wa karibu wameolewa na wengine wana watoto. Jambo hili limekusononesha na kukuumiza sana. Umekuwa mwaminifu kwa Mungu siku zote ukimtumikia kwa bidii. Umefunga, umelia na umeomba sana lakini ni kama Mungu hasikii. Umeanza kukata tamaa ya kuolewa na unatafuta mtu tu uzae naye.

Usikate tamaa wala kuvunjika moyo. Mungu hajakuacha wala kukusahau, anasikia kilio chako na yupo nawe kukupa maisha bora. Hilo ni jaribu lako ambalo ameruhusu upitie maana anajua utalishinda. Mungu alijivunia sana mtumishi wake Ayubu, na aliruhusu shetani amjaribu maana alijua lazima atashinda. Tambua kuwa Mungu anajivunia sana uaminifu wako.

AYU. 1:8
“Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.”

Lazima usimame kwa uaminifu katika jaribu lako ili utoke kwa ushindi. Endelea kumkumbusha Mungu na kumtumikia ukitambua kuwa siku moja utashinda na utamshangilia Bwana kwa ushindi. Bwana atarejeza siku zako zote ulizokuwa unakesha ukilia na kuomboleza.
YOE. 2:25
“Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.”

Siku utakayoolewa hutakumbuka tena kilio chako, itakuwa ni furaha na shangwe pale utakapomngoja Bwana na kulishinda jaribu lako bila kumkosea Mungu. Mungu akakupa maisha yenye furaha na amani na ushindi, zaidi ya uliyonayo sana. Simama katika neno la Mungu, simamia imani yako na usikubali shetani akutoe kwenye mpango wa Mungu.

AYU. 42:12
“Basi hivyo BWANA akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake;”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s