Msamaha Katika Ndoa – 1

Uchungu, kutokusamehe na kisasi ni sumu ya kuua kabisa ndoa. Mwenzi wako anaweza kukutendea mambo ambayo yameumiza sana moyo wako na yeye akawa mgumu kuomba msamaha, hali hii inajenga uchungu kwa yule aliyekosewa. Au pale anapokuwa anakosa anaomba msamaha anarudia anaomba msamaha anarudia na inakuwa hivyo kila wakati. Hii inaweza kuzaa kisasi maana anayetendewa naye atalipiza kwa namna nyingine ili na mwenzie naye aone maumivu yalivyo.

Pia pale mmoja anapokuwa na matarajio fulani kutoka kwa mwenzie na hali ikawa sio bila sababu ya kueleweka. Hii husababisha uchungu ndani ya yule anayetendewa ndivyo sivyo. Inaweza kuwa ni matendo, maneno ya kuvunja moyo na kukatisha tamaa, kutosimama naye hasa kwa ndugu,n.k.  Na wengine hutendewa mambo ambayo wanashindwa kabisa kusamehe hata wakiombwa msamaha maana yamewajeruhi sana sana.

Hali hii husababisha ndoa kuwa kavu, kukosa mapenzi na mahaba na wanandoa huishi kama housemates au wazazi wenza na hisia za mapenzi hufa kabisa. Wengi walio katika ndoa yenye matatizo haya hukata tamaa na kuona kama hakuna tena tumaini na hawatafurahia tena furaha ya ndoa… Tumaini lipo na tutaangalia nini kifanyike sehemu ya pili ya somo hili…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s