Msamaha katika Ndoa – 2

Baada ya kuona jinsi kutokusamehe na uchungu vinavyoharibu ndoa na chanzo chake sasa tuangalie ni jinsi gani unaweza kuponya ndoa ya aina hii. Kwanza lazima utambue kuwa kusamehe ni uamuzi (forgiveness is a choice). Maumivu yanaweza kuwa ni makubwa sana lakini wewe unauwezo wa kuchagua kusamehe. Hii sio rahisi kibinadamu hivyo mshirikishe Mungu katika kila hatua. Mueleze ulivyoumizwa na omba neema ya kusamehe na kuachilia na uamue kuachilia kweli.

Pili amua kutenda matendo ya upendo. Azimia kumtendea mwenzi wako matendo ya upendo hata kama unaona hastahili. Mtendee matendo ya upendo kwa moyo uliochangamka na bila kisasi. Usiangalie kwamba nani mshindi, nani anastahili hili bali angalia kuwa ndoa yenu inahitaji amani na furaha, lazima mmoja ajishushe, ajisacrifice na aamue kuleta tena furaha. Kumbuka hisia za mapenzi zinaweza kupanda na kushuka lakini upendo haupaswi kushuka hata kidogo. Upendo ni uamuzi na upendo wa kweli husamehe saba mara sabini hata bila kuombwa msamaha. Pia usiweke matarajio makubwa kwa mwenzi wako wala usitake mwenzi wako awe kama character fulani wa kwenye movie, mkubali jinsi alivyo na uchukuliane naye kwa upendo.

Tafakari mistari hii kwa kina, usisome kwa mazoea na amua kuitendea kazi.

1 KOR. 13:4-7
“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.”

Advertisements

2 thoughts on “Msamaha katika Ndoa – 2

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s