Wewe ni Baraka au Tatizo?

Dorcas alipofariki mji ulitahayari. Wajane walikusanyika wakilia na kuomboleza kwa kuwa alikuwa msaada mkubwa kwao na aliwajali. Walituma watu wakamwite Petro na alipokuja walimuonyesha nguo alizokuwa amewashonea. Hatusomi kuwa dorcas alikuwa tajiri, bali alikuwa tayari kukutumia kipawa chake kuwasaidia wenye uhitaji.

Je unatumia vipi vipawa na nafasi uliyonayo kwa ajili ya kuwasaidia mwenye uhitaji? Je watu wanaokuzunguka wanakuona kama baraka au tatizo? Sio kila mmoja atakuwa anahudumia wajane, Mungu ametupa maeneo tofauti ya kuhudumia, Simama katika nafasi yako na umtumikie Bwana kwa uaminifu. Siku hizi utakuta mtu akutaka kutoa msaada basi hadi awaite waandishi wa habari na aweke picha kwenye blogs. Sio mbaya kuweka picha lakini mkazo usiwe kuonekana bali kusaidia hasa pale ambapo hakuna anayekuona zaidi ya yule anayesaidiwa.

MDO 9:39
“Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu , wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s