Penda kwa Moyo na Akili Pia

Narudi tena kwa wasichana. Msichana ukiingia kwenye mahusiano nenda na akili zako. Wengi wakishapenda wanaacha akili nyuma wanaenda na moyo tu na kuufuata kila unachotaka, mambo yakiharibika ndipo hukumbuka akili na kuirudia.  Unakuta mdada yupo kwenye mahusiano, akapata safari ya kazi, au akachukua nssf yake baada ya kuacha kazi, hela yoote anamkabidhi boyfriend aliyemwambia kuwa ana business idea anataka kuifanyia kazi na ili kuonekana mstaarabu haulizi wala hiyo business ni ipi.

Siku akiona kimya akiuliza yule kaka anamruka na mahusiano yanaisha, au baada ya kupewa hela kaka anaota mabawa ukimtafuta kila wakati yupo busy. Hapo ndipo msichana anakumbuka alipoiacha akili yake, anajilaumu kwa kuwa mjinga na anaapa kutorudia tena. Akimpata mwingine anasahau yote, anaacha akili na anaenda na moyo. Huyu naye anamdanganya kuwa atamuoa, anampa mimba na kumtelekeza, hapo tena anakumbuka akili yake na anajilaumu na kuapa kutorudia tena. Kwa sababu hii wengine wamejikuta wameingizwa kwenye ulevi, utapeli ba hata utumiaji wa madawa ya kulevya sababu ya kuacha akili na kuingia kwenye mahusiano na moyo pekee.

Penda kwa moyo, kwa akili na kwa mali. Kumbuka yote matatu yanaenda pamoja, ukiacha moja njiani ujue ni lazima utakwama na kulazimika kurudi kulichukua.
Take care ladies, you are so special…

Advertisements

6 thoughts on “Penda kwa Moyo na Akili Pia

  1. Magreth mbona umeongelea side moja tena kwa upendeleo?au unajifanya hujui kuwa wakaka wengi ndio wanaibiwa hela na wadada??..miaka nenda miaka rudi wakaka ndio wanagharamia then mwisho wa siku mdada anatoweka na kumuacha mkaka hana pa kushtaki.

    Pia ukumbuke biblia inasema enyi waume WAPENDENI wake zenu na wanawake WAHESHIMUNI waume. So kibiblia wanawake hawapendi bali sisi wanaume ndio tunaopenda na tunapenda kutoka moyoni ndio maana unaona hata kina mfalme Daudi alipenda hata akamuua askari wake Uria.

  2. Asante, kama wewe ni msomaji wa hapa utagundua kuwa huwa naongelea pande zote kwa usawa maana lengo ni kujenga na kuelimisha na kamwe si ushabiki. Upendo ni kwa kila mtu ndio maana kitabu cha wakorintho 13 kinaelezea upendo una tabia zipi. Ubarikiwe.

  3. Maana kwamba uwe tayari kumsaidia mwenzio kifedha pale anapohitaji na sio kufanya hivyo bila kutumia akili. Ubarikiwe

  4. asante kwa ufafanuzi Magreth lakini wakorintho 13 inazungumzia upendo wa Agape. Upendo wa uchumba/ndoa ni zaidi ya upendo wa agape..ni kama vile kusema upendo wa agape ni subset ya upendo wa ndoa!.na huu ndio upendo ambao wanaume wanakuwa nao na si wanawake…ndio upendo ulioandikwa mwanaume atamuacha baba na mama yake na kuambatana na mkewa; mume atampenda mkewe na mke atamheshimu (si kumpenda) mume!

    Joe

  5. In addition upendo wa Agape una-exist kati watu wote…si upendo wa mapenzi ndio maana upendo wa agape una-exist kati ya dada na kaka!..but upendo wa mchumba/mke ni zaidi na haupo kwa kila mtu…wanawake sana sana wanaweza kuwa na wivu kwa waume zao na si upendo…upendo wa waume kwa wake ni mzito sana unaweza hata kuua ukiingiliwa….usichezee kabisa upendo walionao waume kwa wake zao..ni zaidi ya hatari aiseee

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s