Baraka za Mungu Zimetuzunguka

Shalom, kuna wakati katika maisha yangu nilikata tamaa sana. Mambo mengi yalienda nisivyotarajia, mipango yangu ikakwama na sikuona mafanikio. Nikawa naangalia jinsi nilivyoshindwa na nikakata tamaa sana. Nikiangalia wenzangu wapo mbali kwa yale niliyoyaona ya muhimu na ndio mafanikio, nikaona kama Mungu amenisahau na nafsi yangu ikainama sana.

Nikamlilia Mungu, kwanini umeniacha? Kwanini unanipita unapozuru wengine? Kwanini zamu yangu haifiki? Hapo ndipo Mungu alinifundisha kitu kikubwa, baraka zake zimetuzunguka kila upande ila tatizo sisi huangalia tusivyonavyo na fursa tulizozikosa na kulia sababu ya hayo na kutokuona baraka alizotupatia na fursa tulizonazo. Hapo nikageuza mtazamo wangu, nikagundua Mungu amenibariki sana sana, na fursa nilizonazo ni nyingi kuliko zilizopotea. Nikawa mtu mwenye furaha zaidi, aliyejaa shukrani na kwa hakika nimemuona akizidi kunibariki.

Leo nakutia moyo, haijalishi unapitia nini wewe usikate tamaa. Mwangalie Mungu maana hakika utakwenda kumsifu maana atakuonyesha alivyo mwema na aliye afya yako. Usiangalie yale uliyoyakosa, tazama yale uliyobarikiwa na muombe Mungu akuonyeshe fursa ulizonazo.

ZAB. 42:5
“Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s