Fufua Wazo Lako…

Umekaa ukamuomba Mungu kwa muda mrefu akupe wazo la biashara au huduma ambayo kwa hiyo kusudi lake kwako litatimia. Umepata wazo na unaamini kabisa limetoka kwa Mungu. Sababu ya ubinadamu unatafuta ushauri kutoka kwa mke/mume, rafiki, wazazi, ndugu n.k. na inatokea wanakukatisha tamaa kuwa “hutaweza, wewe huna hiki au kile, hilo jambo wanaliweza kina fulani, acha ndoto za mchana n.k.”. Baada ya kusikia hivyo unavunjika moyo unaliacha na kuendelea na mengine, lakini jambo hili bado linaimba ndani yako.

Simamia maono yako! Usikubali hofu au mashaka ya mtu mwingine yakufanye ushindwe kutimiza kusudi la Mungu katika maisha yako. Wewe ndiwe Mungu amekupa jambo hilo, anajua kuwa unaweza na utafanikiwa. Watu waliotuzunguka ni wa kutupa ushauri ila maamuzi yanabaki kwetu baada ya kuangalia faida na hasara. Usiogope kushindwa kabla hujajaribu, je unajuaje kama utashindwa? Na hata ukishindwa hilo somo utakalojifunza baada ya kushindwa huwezi kulipata kwa kutokujaribu.

Wengi hapa mna mawazo mazuri lakini mmeyafungia kwenye note book baada ya mtu fulani unayeona kafanikiwa sana kakuambia haiwezekani. Leo nakutia moyo, unapoanza robo ya mwisho ya mwaka huu azimia kufufua lile wazo lako ambalo umelizika. Usikubali mwaka huu upotee bila kufanya kitu kuhusiana na wazo lako. Anza sasa na Bwana Yesu yupo pamoja nawe.

Advertisements

One thought on “Fufua Wazo Lako…

  1. Mungu akubariki sana yaani umegusa hasa moyo wangu niko nina wazo muda mrefu ili niweze kumtumikia Mungu kwa nafasi kuliko sasa ila nilikuwa nalikatia tama kutokana na ushauri wa watu. WIki iliyopita nimekuta tangazao nikaandika nami plan yangu, kutokana na ushauri wako huu nitasimamia wazo langu hili kwa maombi na kulikiri hadi litimie, Yeremia 32:26-27. Barikiwa sana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s