Matarajio kwa Msaidizi wa Kazi

Wanawake mara nyingi tunakuwa na matarajio makubwa sana kutoka kwa wasichana wa kazi kuliko uwezo wao. Ni vyema tukiwaelekeza kwa utaratibu na upole, ukiangalia ni mambo gani muhimu anayopaswa kufanya kwa ukamilifu na mengine wewe unamalizia pale aliposhindwa. Kumbuka msichana huyo kwanza kiumri ni mdogo, wengi wao elimu ni ndogo sana hivyo uwezo wa kufikiri haraka ni mdogo, exposure pia ni ndogo hivyo multitasking inahitaji mazoezi ya kutosha. Mpangie kazi unazojua atamudu na atafanya kwa ukamilifu kwa kila siku na nyingine awe anafanya mara moja kwa wiki kama kufuta madirisha, kufua mashuka n.k. siku ambayo wewe upo nyumbani.

Wanawake huwa tunakosea sana, tunasahau kama kazi za nyumbani ni nyingi sana na zinachosha sana unaporudi na kukuta kitu kidogo tu hakipo sawa basi unakuwa mkali kupindukia. Lakini akikuachia nyumba na watoto siku moja akienda kusalimia kwao jasho linakutoka. Tutambue mchango wa hawa wasaidizi, tuishi nao kwa utu na kuwajali. Anapokosea kidogo tambua naye pia ni mwanadamu chukuliana naye kama mwanao na utaona jinsi atakavyojituma na kuishi vizuri na wanao.

Advertisements

One thought on “Matarajio kwa Msaidizi wa Kazi

  1. asante kwa topic nzuri dada. Swali langu ni moja kwann wamama wa tz wanapenda kuwa na ma-housegals wakati wenzao wa nchi za ulaya&america hakuna mambo kama haya??je ni uvivu au ubwanyenye?

    maana ukisema kuwa ni sababu ya kazi itakuwa si sawa..hakuna wanawake wanaofanya kazi kama wa ulaya tena pasipo kuzuga kazini maana mtu unalipwa kwa masaa ya kazi unayofanya no kuchelewa no excuses! na bado utakuta wanawake hao wana familia na watoto wadogo. Pia tusiende mbali sana hata wamama wa hapo tz vijijini nao husikii habari ya housegals..wao wanalima (na hata mtoto mgongoni), wanakwenda umbali mrefu kuchota maji,kukata kuni,kupika,etc. Je kuna nini na wamama wa mjini hasa wa hapo darisalama?

    Labda uje na mada ya jinsi ya kupanga muda (time management) na kuondokana na huu utegemezi wa ajabu wa mahousegal..pia nadhani ni dhambi kubwa sana kwa jinsi wamama (hata walokole) wanavyo watreat hawa mahousegal kwa kuwalipa mshahara ambao ni chini ya kima cha chini, hawana mapumziko ya week wala likizo ya mwaka, overtime allowances, kuwanyima fursa ya kujiendeleza kielimu kama watu waliokatika kazi nyingine, kuwaachisha masomo watoto ambao walitakiwa kiumri wawe shuleni, etc etc..sijui dhambi hii kubwa wanayowafanyia wataponea wapi siku ya hukumu!

    Changamoto kubwa ni kwanini wa nchi nyingine wanaweza but wa darisalama hawawezi..tena utakuta mama wa ulaya anatoka sokoni amebeba mizigo bado yupo anasukuma kigari cha mtoto na kupanda mabasi bila kuwa na housegal. Tafakarini!

    sam

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s