Je ni Lazima Kuwa na Wasichana wa Kazi?

Baada ya jana kutoa mada ya wasichana wasaidizi wa nyumbani, kwenye blog kuna mtu amekuja na swali lifuatalo na tulijadili kwa pamoja. Anauliza ni kwanini wanawake wa Tanzania tunategemea sana wasichana wa kazi na hatuwezi kuishi na kuangalia familia zetu wenyewe bila wasichana wa kazi. Mbona nchi za ulaya hawana wasichana wa kazi na wanafanya kazi na kuwalea watoto wao wenyewe? Mimi sina majibu, nasubiri nisikie toka kwenu. Tulichambue kwa kuangalia pande zote, uhalisia wa maisha na malezi bora kwa watoto wetu. Karibuni.

Advertisements

8 thoughts on “Je ni Lazima Kuwa na Wasichana wa Kazi?

 1. Shalom wapendwa,
  mimi pia ni mama mfanyakazi na nina msichana au maid ananisaidia kazi.
  Nianze mimi nilivyolelewa mama yangu pamoja na kusoma baba aliomba akae tu nyumbani asimamie familia. Watoto tulikuwa 7 na tuliongozana kwa maana tulipishana wengine mwaka na nusu na wengine miwili na tulikuwa tunasoma. Mama alihitaji msichana kwani ni familia kubwa ingawa na yeye nakumbuka alikuwa akipika na hata kufua sambamba nao. Lakini nakumbuka kulikuwa na vitu vingi vya kumsaidia: gari na dreva na foleni zilikuwa hamna kusema ameenda hospital au sokoni atawahi kurudi nyumbani. Maisha yalikuwa ya amani na kujitosheleza kipato hata kama mzazi mmoja alikuwa anakaa nyumbani tu sana anajishughulisha na mifugo kidogo tu.
  Sasa hivi hali ya maisha imepanda juu mno, wakati mimi na ndugu zangu tumesoma bure kuanzia primary hadi chuo au kwa gharama ndogo sasaivi fees za watoto ni balaa, kodi au ujenzi juu, matibabu, usafiri nk. Inabidi wazazi wote wafanye kazi tena sio ndogondogo kwa kina mama bali fulltime na kwa foleni na usafiri wa shida majiji yetu mnajikuta wote mnatoka saa 12 mnarudi sa 12 hadi saa 1 usiku: nani aangalie watoto? aandae chakula cha watoto na kuwafulia? afanye usafi wa nyumba maana hii saa 1 usiku kuanza usafi na ujiandae uamke saa 11 asubuhi? Wenzetu huko nchi zilizoendelea wako mbele wana daycare, usafiri wa uhakika, mashine za kufulia na wengi hutumia take away food au kutayarisha chakula na kuhifadhi kwenye mafridge jioni akipitia wanawe anapasha tu, vyombo nguo ni mashine zinasaidia. Kingine mgawanyo wa kazi za nyumbani ni sawa kwa wanandoa wote. Huku kwetu hata akitoka saa 10 baba akifika anajinyoosha anamsubiri mama aje apike sana amesaidia homework ya watoto wengine anaishia kijiweni au kutembelea ndugu, rafiki au kwenye huduma hadi saa moja au mbili ndo anaonekana nyumbani. Kwa karne hii mwanamke yeyote Mtanzania aliye na familia na anajishughulisha anahitaji msaidizi. barikiweni

 2. Wenzetu kule Ulaya wao wanaweza kuamua kwamba akishazaa mtoto kukaa nyumbani na kulea mtoto mpaka umri wa kwenda shule ndio wanarudi tena kazini. Na kitu kingine wenzetu wanaweza kuamua afanye masaa manapi kwa siku au kwa wiki. Sisi huku ni tofauti ukishaacha kazi kupata kazi tena inakuwa vigumu sana.

 3. Nimekusoma rosemary na uko sahihi to some extent lakini ukumbuke daima excuses and not facing a challenge si njia nzuri!.

  wel kuhusu suala la kuwa na machine ya kufulia kama ulaya nadhani si ishu kubwa kama ukijipanga maana gharama za kumuajiri mfanyakazi, malazi, matibabu, mavazi, etc kwa mwaka ni kubwa mara dufu na bei ya kununua hiyo machine ambayo unaweza kuitumia kufua mara moja tu kwa week kwa nguo zote (maana unaweza sema kufua mara nyingi tabu umeme unakatika katika).

  Umezungumza vyema upishi wa chakula kabla endapo unachelewa kurudi. Kuna mfano mmoja mama mzee hapo dar aliwahi kuniambia hajawah kuwa na housegal maisha yake yote maana yeye hupika chakula cha kesho yake usiku au asubuhi sana na kukiweka vizuri kwenye fridge hata mume wake & watoto wakiwahi kurudi wanapasha moto na kula kama watachelewa. Wamama wa mjini mna kila kitu majiko ya kuivisha haraka, oven za kupashia moto,etc ambapo mapishi hayachukui hata zaidi ya saa moja kuivisha chakula kuliko wa vijijin ambao inabdi kwanza wakatafute kuni. Narudia kama utaamua kuinvest vizuri once kwenye gharama za kununua jiko zuri (umeme/gesi),etc ni cheap kuliko gharama za housegal na dhambi zinaso-associate na treatment unayompa!

  Mgawanyo wa kazi kati ya mume na mke inategemea sana na initiative anayofanya mama…mfano kama mama ukipanga vitu vyote hivyo na kumweleza mume madhara ya kuwa na housegal hakika mume lazima by default atakuwa anasaidia kazi ndogondogo…wanaume tumeumbwa ku-act accordng to situation sasa kama naona nina wamama wawili ndani (mke&housegal) lazima nitashinda kwenye tv maana haiwezekani wamama wawili wakashindwa kufanya kazi at the same time.

 4. lilian umesema vyema kuhusu kulea mtoto hadi anakwenda shuleni…vp basi kwanini labda usiwe na housgal kwa kipindi kifupi letsay miaka mitatu hadi mtoto anapoanza shule then baadae ukarudi kufanya kazi zako mwenyewe bila housegal??

  hiyo ya kuamua kufanya kazi kwa masaa mangapi kwa walio ulaya si kweli kwa maana ya kufanya masaa machache…kwa week wengi wanalazimika kufanya masaa 40 hadi 50 ili kuwa na pesa ya kumudu kulipa bills otherwise hawata weza kuishi..!

  me bado nadhani ni kutopenda kufanya kazi, uvivu, ubwanyenye, etc ndio sababu kubwa ya kuendekeza ma-housegal. Ndio maana siku hizi utakuta watu wanaoana tu hata hawajapata watoto tayari wana housegal..na wengine wakisha kuwa nao wanaongeza housegal hadi wawili.!.utakuta pia mfano mtu hata kuosha gari lake lazima atafute mtu amlipe ili kumuoshea wakati maji,sabuni&mikono anayo!au hata kukata majani/michongoma/kupiga rangi chumba/etc….huku ulaya huu upotevu wa pesa hakuna!.

  ukweli ni kuwa familia nyingi zinapoteza pesa nyingi na kuchuma dhambi kubwa (kwa dhuluma wanayofanyiwa housegals) kwa huu uvivu wa kuendekeza na hakika kama mtu ukiamua kuacha&kubadilika utaweza!.muhimu ni kujua kupanga muda vizuri maana haiwezekani mtu kila siku unatumia zaidi ya masaa mawili kutazama tv na kutegemea mabadiliko.

  sam

 5. Sam naona huelewi mazingira niliyoongelea yanachangiwa na uwepo wa uhakika wa umeme na kipato pia. Wengi tumeweza kununua fridge lakini hata tuwe na hizi electric na gas cooker bado hatumudu kuzitumia mwezi mzima pia uhifadhi wa vyakula kwenye fridge inahitaji umeme. Kusema kweli mimi msaidizi ninaye mmoja tu na kazi yake maalumu ni mifugo na vile ninakaa naye basi hupika na kufua lakini jumamosi na jumapili ninapokuwepo namruhusu aende kwa familia yake ni mke na mama wa watoto 4 hata nikiwa leave simhitaji, tatizo ni ulinzi huwezi acha nyumba pekee kupishana muda wa kazi na shule watoto wanatangulia na pia safari kazini. Ukiisha muachisha mtu halafu aende kupata kwingine kuja kupata mtu mzuri kazi sana na wao kumbuka wana shida na wengi wanategemea mshahara huu tu kuwaachisha sijui ukisafiri au kuumwa uhitaji mtu huwezi kupata mtu mzuri kwa ghafla. Sijui kwa wengine lakini sisi tunaishi nao kama ndugu, tunawasomesha na kuwasaidia mitaji au ujenzi na mwisho wa siku wafanyakazi hawa walioondoka wamekuwa kama sehemu ya familia au ndugu.

 6. sawa dada rosemary kama unayafanya kwa hakika na kweli ya kumuogopa Mungu maana kwa utafiti wangu mdogo manyanyaso wanayopewa hao ma-housegal tena na wamama waliookoka ni makubwa sana huku wenyewe wakiona ni sawia machoni pao wenyewe!

  Ni vizuri na inampendeza Mungu kama mama umeshindwa kufanya kazi zako mwenyewe na kushirikiana na mume ukawa unamtendea haki housegal na si kwa kiwango cha machoni pa watu au kwa shida ya alikotoka bali kwa kiwango cha haki mbele ya Mungu mfano kuwa na mkataba nae wa kazi, kumlipa mshahara halali wa kima cha chini wa serikali kwa sekta binafisi, kumpandishia mshahara atakapokuwa anazidi kukutumikia kwa miaka, kumpa job description na masaa ya kazi, kumlipa overtime kama atafanya masaa zaidi, kumpa mapumziko ya week na likizo za mwaka, kumlipia ppf/nssf, bima ya afya, kumlipa mshahara tarehe kamili, kumuendeleza kielimu, kumkubalia kwa amani atakapotaka kuacha kazi au kumlipa mshahara kama utamfukuza kwa makubaliano iyaliyopo kwenye mkataba!

  Endapo unamfanyia housegal kinyume na baadhi ya niliyoyataja hapo juu hata kwa kisingizio cha kuwa anatoka familia maskini, anahitaji sana kazi, ninachompa (kidogo) kinamtosha sana, etc ujue kuwa ni DHAMBI KUBWA MBELE ZA MUNGU hata kama kwa wanadamu au machoni pako mwenyewe unaona uko sahihi. So hata kama ni mlokole sana ujue hakika utajibu mbele za Bwana siku ya mwisho. Kuwa na housegal ni gharama sana ndio maana nchi nyingine wanashindwa kuwa nao si kwakuwa hawapendi bali ni kuwa wana-hofu na Mungu ya kuwa-treat vibaya housegals na hakika Mungu ata/ana-walipa hata kama si walokole wa kwenda makanisani!

  sam

 7. Ahsante sana kaka Sam, Mungu atusaidie, pia ni jukumu la wote, baba na mama kwa hayo uliyosema na si mama peke yake. watumishi wa ndani wanahitaji haki katika kulipwa ujira wao hata Mungu amelisemea sana hilo kwenye bible.
  Dada Rosemary nakubaliana na wewe kumaujiri mtu wa part time kufanya kazi kama za kufua, garden na usafi mazingira, lakini nyingine ni wajibu wa mke kuzipangilia na familia yake kufanya.
  Watoto wetu pia wakifika hata miaka 6 ni vizuri tukawafundisha kazi kama kujifulia wenyewe nguo zao, kujifanyia usafi vyumbani mwao, kupika etc ili kupunguza cost za kuajiri watumishi wa ndani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s