Mwanaume na Shughuli za Nyumbani

Wakati tunakua nakumbuka mama wengi walikuwa wanatoka kazini saa nane hadi kumi au wengine wanajishughulisha na kilimo, ufugaji na biashara hapo hapo nyumbani. Hivyo ilikuwa ni kawaida baba kurudi kazini, kupata chai ya jioni, kunyoosha miguu akisoma gazeti kusubiri chakula cha usiku. Ilikuwa nadra sana kumuona baba akihangaika na watoto, mifugo, bustani au mambo mengine ya nyumbani.

Siku hizi maisha yamebadilika, mama na baba wote wanaondoka nyumbani alfajiri na kurudi usiku na mara nyingine baba anawahi kurudi kuliko mama. Hapa inahitajika busara sana jinsi ya kuangalia mambo ya nyumbani. Yupo msichana wa kazi atapika na kufanya usafi, ila baba utambue kuwa unajukumu pia pamoja na mke wako la kusimamia homework za watoto wako, kuangalia kama amekula vizuri, kumbembeleza ili alale, na kumsaidia mkeo mambo madogo yenu binafsi kama kuandaa nguo za kazini, n.k kulingana na uhitaji. Sio unatoka kazini unapitia kijiweni kuongea tu na wenzio, familia ni yako na unajukumu ya kuwepo na sio tu kutoa hela.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s