Maombi ya Kufunga Kwa Ajili ya October

Leo ni Siku yetu ya Maombi ya Kufunga.
Maombi haya ni kumkabidhi Mungu mipango yetu yote ya mwezi huu wa kumi, kumweleza yale tunayohitaji atufanyie na kutufanikisha na kuomba ulinzi wake kwetu na familia zetu. Muombe aongoze hatua zako, mawazo yako, mipango yako na maamuzi yako yote. Akupe kibali cha kiungu (devine favour) katika kila utakachokifanya. Najua alfajiri umeomba, mchana tafuta muda hata kama ni hapo kwenye meza yako ofisini uombe na jioni utamalizia kuomba ukifika nyumbani. Tafuta notebook uandike haya maombi yako ili pale Mungu atakapokujibu uweze kumpa shukrani.

MIT. 16:3, 9
“Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.    Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.”

ZAB. 37:5, 18-19
“Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.    BWANA anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.    Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.”

Advertisements

4 thoughts on “Maombi ya Kufunga Kwa Ajili ya October

  1. Bwana Yesu Asifiwe sana, Nashukuru sana kwa kunikumbuka ila nimechelewa kupata hii mail. Nauliza je itakuwa vibaya nikifanya haya maombi leo. Aksante sana.

    ________________________________

  2. Usiwe na shaka, Bwana anaangalia nia iliyo ndani ya moyo wako hivyo ni sawa kuomba leo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s