Wiki hii ni wiki ya kumtafuta Mungu. Kutafuta kulijua kusudi lake katika maisha yetu, kuyatambua mapenzi yake na kuamua kuishi kuzifuata sheria zake. Ni wiki ya kujiweka wakfu kwa Mungu, kumtafuta kwa bidii. Mambo mengi yanakwama katika maisha yetu sababu hatujampa Mungu nafasi anayostahili. Badala ya yeye kuwa usukani wa maisha yetu amekuwa spare tire, kwamba hatuna habari naye hadi pale mambo yanapoenda mrama. Sasa wiki hii ni ya kutambua kuwa Mungu ndio kiongozi wetu na kumtafuta kuwa naye siku zote za maisha yetu.
1 NYA. 28:9
“Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.”