Kusamehe Kutakusogeza Karibu na Mungu

Kumtafuta Mungu kunajumuisha kuwasamehe wote waliokukusea, kuachilia na kusonga mbele. Kusamehe haimaanishi kuwa hawajakosea, bali inaonyesha ulivyokomaa kiroho, upo tayari kuanza ukurasa mpya na kuiweka nafsi yako mbali na visasi. Kutokusamehe, hasira na visasi humfanya mtu kuonekana mzee, kukosa uchangamfu, kupata magojwa ya moyo na kushindwa kufanikiwa sababu hawezi kuconcentrate.

Kusamehe kuna faida nyingi sana kwa anayesamehe hasa pale unapoamua kusamehe bila hata kuombwa msamaha na kusamehe yale ambayo kibinadamu hayasameheki. Siwezi kukudanganya kuwa kusamehe ni rahisi na huja automatically, si kweli. Tena kusamehe mtu wa karibu uliyemwamini na kumpenda akakutenda ni ngumu sana kuliko kumsamehe mtu unayefahamiana naye juu juu. Kusamehe ni uchaguzi, na ni uchaguzi wa kujitoa hasa. Ni uchaguzi utakaokuweka huru na kukusogeza mbele za Mungu. Ni uchaguzi utakaosababisha Mungu asikie maombi yako na kukusaidia. Ni uchaguzi ambao wewe mwenyewe ndiwe mwenye uwezo wa kuufanya. Usikubali watu wakushawishi kutokusamehe, ni wewe unayeumia ndani na sio wao. Amua kusamehe sasa na anza maisha mapya bila mtu yoyote ambaye hujamsaheme. Ni ngumu ila Inawezekana!
 

Advertisements

4 thoughts on “Kusamehe Kutakusogeza Karibu na Mungu

  1. Bwana Wetu Yesu KristoAsifiwe!!!!! Nashukuru kwa neno zuri namwomba Mungu wa rehema anisaidie niweze kusamehe na kusahau moja kwa moja

  2. nahitaji nguvu ya Mungu kumsamehe mume wangu…..anarudia kosa lile lile!roho inauma ila maneno ya leo yamenibariki

  3. Swala la kusamehe ni gumu kwa kweli, tena pale mtu anapokuwa anarudia kosa lile lile. Tunahitaji neema ya Mungu ili tuweze kujua MUNGU anatuhitaji tufanye nini kwa wakati huo. Ubarikiwe sana.

  4. Mimi nahisi nimesamehe ila simhitaji kuwa karibu nae tena ila anapokuja ok asiponitafuta sijisikii kumtafuta je ni kosa? mimi sitaki ukaribu naye tena maana alikuwa rafiki yangu sana familia zetu tunajuana ya ndani kabisa ila yeye akikaa na rafiki zake wengie hunisengenya hadi basi. nimemsamehe na ninamwomba mungu nisimkumbuke tena.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s