Mjengee Mtoto Misingi Mizuri

Wazazi afya za watoto na ufanisi wao shuleni unategemea sana malezi yetu na ratiba za nyumbani. Ili mtoto awe na afya njema na kuweza kumsikiliza mwalimu darasani vizuri na kuelewa ni lazima awe amekula mlo wenye afya na kulala kwa muda wa kutosha. Ni lazima watoto wale mlo kamili wenye virutubisho vya kutosha na sio kila siku junk food, juice za mabox na biskuti. Mzoeze mtoto kula vyakula vyenye afya hasa mboga na matunda na mtengenezee juice natural na sio za viwandani.

Pia muda wa kula hasa chakula cha usiku ni wa muhimu sana. Mtoto asile zaidi ya saa mbili usiku yani mbili kamili hivyo muda wa kula ni saa kumi na mbili na saa moja basi. Na baada ya hapo anacheza au anafanya homework na saa mbili na nusu hadi tatu ni muda wa kupiga mswaki na kulala. Mtoto anaenda shule saa kumi na mbili asubuhi, hadi saa nne hajalala hivi unategemea atamsikiliza mwalimu kweli na unakuta amekula saa tatu usiku.

Mjengee mtoto utaratibu mzuri na utamsaidia sana maana atakuwa hivyo na ataweza kupangilia muda wake maana kazoezwa kuishi kwa mipango. Ijumaa na jumamosi anaweza chelewa kulala maana haendi shule kesho yake ila kula isiwe zaidi ya saa mbili kila siku.

One thought on “Mjengee Mtoto Misingi Mizuri

  1. dada yangu huyo ni mtoto wa miaka mingapi??akilala mapema atafeli jamaniii na elimu yenyewe ya kibongo tight sana….mbona dada ww ulikuwa unapiga msuli hadi saa saba usiku??au kipinde kile haukuwa mtoto??ha ha

    mtoto-mkubwa John

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s