Simama na Mwenzi Wako

Ni muhimu sana tena ni lazima kusimama na mwenzi wako inapotokea kupishana maneno kati yake na ndugu yako/zako. Mwenzi wako amewafahamu na kufahamika na ndugu zako sababu yako, wewe ndiwe mwenye jukumu la kuhakikisha havunjiwi heshima wala kudhalilishwa nao kwa hali yoyote. Usiruhusu kamwe ndugu zako wamseme na kumsimanga mwenzi wako eti hana hela, mbahiri, mchoyo, mbaya, hazai, n.k. Lazima uweke mipaka na ndugu wote wajue kuwa mipaka yao imaishia wapi na watambue kuwa utasimama na mwenzi wako katika hali zote siku zote.

Biblia inasema mwanaume atawaacha baba yake na mama yake na ataambatana na mkewe ila kwa kweli ni wanaume wachache sana wanaofanya hili. Wengi wanasahau kuwa wakuambatana naye ni mke badala yake wanaambatana na mama au dada na kumuacha mke akisumbuka na kutokupewa nafasi yake. Mambo haya yameleta migongano sana kwenye ndoa. Kumbuka sio wazazi wala ndugu waliompenda mume/mke wako kwanza, ni wewe uliyempenda na kisha kumtambulisha kwao. Wewe ndiwe mwenye jukumu la kumpenda na kuhakikisha hakuna anayempa wakati mgumu. Awe hajasoma, hana hela, mbaya, mchoyo na kila watakachokiongea, wewe ndiwe uliyemchagua, hukuyumbishwa na hayo hivyo basi simama naye siku zote.

Advertisements

2 thoughts on “Simama na Mwenzi Wako

  1. Nashukuru kwa ujumbe mzuri, mimi na familia yangu tumefarijika na kujifunza mengi ktk hili.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s