Msichana Usijirahisishe

Shalom
Tunaendelea na somo letu na leo ni maalumu kwa wadada. Wasichana wengi wanalalamika wamepewa mimba na kuachwa na mipango yote na kuolewa imeishia hewani. Hapa naongelea upande wa wasichana na nitarudi kwa wanaume. Msichana tambua hata kama ni kweli unatamani kuolewa kuliko kitu kingine na upo tayari hata iwe leo, kamwe usijionyeshe kwa mwanaume kuwa upo desperate kwa ndoa. Jitahidi sana kucontrol desperation yako ya ndoa ili uweze kufanya maamuzi ya busara na vilevile usisababishe mtu kukutenda na kukuacha na maumivu.

Desperation inasababisha msichana kujirahisisha na kufanya maamuzi ili kumpendeza fulani. Sababu unahitaji sana kuolewa hata akikuambia hamia kwake wewe unahamia maana unadhani kufanya hivyo ndio utamkamata. Kama mwanaume hajaamua kukuoa hata uhamie kwake, uzae naye, umnunulie gari yote hayo hayatabadili msimamo wake na hata akikuoa atafanya tu ili kuishi na mtoto wake lakini upendo hakuna.

Yakobo alikuwa anampenda Rachel, baba mkwe wake akampa Leah badala ya Rachel. Pamoja na yakobo kulala na Leah bado upendo wake ulibaki kwa rahel na alafanya juu chini kumpata na wala upendo haukuhamia kwa Leah sababu amelala naye.

Usijirahisishe kwa sababu unataka kuolewa, hakuna mtu anayetaka kumuoa msichana aliye rahisi rahisi. Wewe ni wa thamani, hakikisha unatafutwa kama Rachel na sio kupatikana kirahisi kama Leah. Utafanyaje?? Rejea somo la jana… Ubarikiwe

Advertisements

3 thoughts on “Msichana Usijirahisishe

  1. Ninackitika sana kwa kuona binti aliyeokoka anapofanya mambo ambayo ni aibu mbele za MUNGU na mambo ambayo ya nampeleka kwenye umauti!inashangaza bt hii ni kutokana na wapendwa wengi kuwa nje ya sheria za MUNGU.So lazima upokee kile ulicho kipanda!eti unataka mume bora thn unakuwa kinyume na maelekezo ya Mungu yaan unafikia hatua unamuonjesha unayemuita mchumba wako ili akuoe!jamani hayo ndiyo maelekezo ya Mungu?BIG NO!Tarajia kupata yule acyekufaa coz atakuwa hajatoka kwa God bt atakuwa ametoka kwa namna ya udhaifu wako na kukaidi sheria ya God!Mungu ametupa ahadi zake na yeye c muongo kama binadamu!Kasema lolote tuombalo kwa imani atatupatia!so mashaka,imani haba, kuchoka ,kukata tamaa n.k kumekufanya kupokea ulichonacho!God katuteli tusikome kuomba yaan tukeshe tukiomba.so haya mambo ya kuhamia kwa mwanaume cjui kumuonjesha kabla ya ndoa ni mambo ya kipepo!Badilika leo dada na ucmame na MUNGU ILI UONE UKUU WAKE NA UONE JINC ACVYO MUONGO KWENYE AHADI ZAKE.UCTANGETANGE BINT CMAMA IMARA NA YESU.GBU

  2. Ahsante kwa ujumbe mzuri dada,ni kweli kabisa wadada tulio wengi tunapenda kujihamisha wenyewe kwa wanaume madai tusipofanya hivyo tutaachika..tunasahau kwamba miaka inazidi kusonga mbele na mwanaume anazidi kukuchoka na kuona wengine,ni rahisi sana kukuacha..Mwaka mpya unaanza tunatakiwa kubadilika na kuthamini utu wengi..Mwanamke ni kiungo sana muhimu katika jamii..Tumuombe Mungu sana..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s