Mke Mwema Hutoka kwa Bwana…

Shalom

Kwanza nianze na vijana wa kiume. Misingi ya ndoa inaanzia kwenye mahusiano, lakini wakaka wengi siku hizi wamekuwa ni wavunja moyo sana. Ukijichunguza kwa makini utagundua ni wadada wengi sana umewavunja moyo na kuwaumiza. Unakuta kijana anaona ufahari kuwachumbia wadada zaidi ya mmoja na kisha kuwatosa, kuwachumbia na kuwatosa na wanapokuwa wanagombana kwa ajili yake anajiona kuwa ni mwanaume.

Leo unaona kama ni mchezo, na kweli wengi wanalia kwa ajili yako umewatosa baada ya kuwapa matumaini, lakini kumbuka apandacho mtu ndicho atakachovuna. Wasichana wanapolia kwa ajili yako umewatenda vibaya, maombi yao yanafika kwa Mungu na hakika atashuka kuwatetea. Kama huna mpango kwa kumuoa kwaninu kumdanganya na kumpa tumaini la uogo? Wengine mnawapanga makusudi kuangalia yupi bora, jamani mke sio bidhaa biblia inasema mke mwema mtu hupewa na Mungu. Acha kuwapanga wasichana badala yake nenda mbele za Mungu naye atakuonyesha yule mmoja ambaye ameandaliwa kwa ajili yako, aliye ubavu wako.

Advertisements

3 thoughts on “Mke Mwema Hutoka kwa Bwana…

  1. asante dada ila hili suala ni tete sana. Je kuna ubaya wa kuachana kabla ya ndoa endapo Mungu atasema na wewe kuwa umekosea katika kuchagua?maana nionavyo bible imeongelea zaidi madhara ya kuachana katika ndoa na si kabla ya ndoa. Kufanya makosa katika kuchaguana nadhani pia si katika karne hii bali hata hapo zamani watumishi wakubwa tu kama Daudi walikosea kumsikia Mungu na wakajirekebisha. Sasa je hata kama ulimpa tumaini la kumuoa msichana na baada yake ukagundua kuwa si wa kwako uendelee tu kwenda kumuoa ili asikulilie hapo baadae?

    Maana pia hili suala la kuonekana kumpa tumaini la uongo ni tata sana na mara nyingi (asilimia kubwa) si kuwa wakaka wanapenda kutoa hili tumaini la uongo bali ni kuwa nia yako na moyo wako na akili zako mwanzoni unaweza kuwa ukahisi umepata mtu sahihi. Je ikitokea kuwa ukaja kugundua kuwa mdada wa watu humfai/hakufai kufunga ndoa nae uendelee nae tu?je kilio cha kabla ya ndoa au baada ya ndoa kipi ni cha hatari zaidi?naomba utuchambulie zaidi hili suala maana japo tunaomba sana lakini saa nyingine tunakosea katika kusikia.

    sam

  2. mimi mwalami nipa dales saram tz namba .tushilikiane kuniombea sina kazi sina mchumba.nahijaji hata reo nipate .vitu ninavyo vihitaji mimi fundi ujenzi .nisaidieni kuniombea.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s