Timiza Ndoto Zako Sasa

Nirudi tena kwa wadada. Bado tupo na somo la mahusiano. Kuna wasichana wanafikiri maisha yao yataanza pale watakapoolewa. Unakuta mdada yupo tu wala hana malengo yoyote na maisha yake, mradi anafanya kazi basi yeye ni kula na kuvaa tu. Maisha unaanza pale unapozaliwa, haihitaji kuolewa ndio uwe na mipango ya maisha. Kuna walioolewa wakiwa na miaka kumi na kitu, wengine, ishirini, thelathini na pia wapo walioolewa wakiwa na miaka arobaini na kitu. Sasa kama unasubiri uolewe ndio uplan maisha yako unakosea sana. 

Lazima uwe na ndoto ni wapi unataka kufika, nini unataka kuwa nacho na kufanya kazi kwa bidii ili kuifikia ndoto yako. Unapoendelea kuitimiza ndoto yako Mungu atakukutanisha na mume wako huko huko na pamoja mtakuwa na mipango ya familia. Kama unandoto ya kuongeza elimu ifuate, iwe ni kufanya biashara, kufungua kampuni, kulima, kuwa muhubiri, muimbaji n.k. anza sasa kuitimiliza ndoto yako na umuombe Mungu akupe mtu ambaye kwa  pamoja mtatimiliza ndoto zenu.

Ukweli ni kwamba, kama sasa upo single na huwezi kuwa na mipango, ndoto na kufanya kazi kwa bidii, utakapoolewa na kuongezewa majukumu ya familia, na utakapopata watoto hutaweza kabisaa hata kuwa na hiyo ndoto. Tumia muda wako vizuri, tumia fedha zako vizuri na tumia vipawa vyako vizuri kuanzia sasa.

Advertisements

2 thoughts on “Timiza Ndoto Zako Sasa

  1. Dada Mage,

    nimeipenda hii hekima sana.

    wanawake tunasahau kuwa Mungu ametuweka kufanya purpose zake nyingi sio tu ya kuolewa. kuolewa ni moja wapo tu.

    Hekima ya Mungu izidi kukufunulia na ufikishe ujumbe kwa wengine

  2. nimeona wanaume wasiotaka kumkuta mwanamke aliye mzidi elimu au maendeleo,hivyo inapelekea wanawake wengi kukaa tu na kusubiri ndoa,ndio waanze maendeleo.Nawashauri wanawake wajiendeleze kwa kadiri watavyo barikiwa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s