Maombi Juu ya Watoto

Watoto wetu wanapitia hatari nyingi sana katika maisha yao. Matatizo ya watoto katika kizazi hiki ni mengi sana nasi wazazi hatuna nguvu ya kuwalinda na hayo yote zaidi ya kumwita Mungu. Wiki hii tunaenda kuomba kwa ajili ya watoto wetu, ajali za majumbani, ajali za shuleni, unyanyasaji wa kila aina, magonjwa, kiburi, utukutu, marafiki wabaya, kutokupenda shule, kushindwa kusoma, nguvu za giza na mengine meeengi.

Tumlilie Mungu kwa ajili ya watoto wetu, na kuwakabidhi mbele za Mungu. Hakuna awezaye kuwalinda na kuwalea watoto bila msaada wa Mungu.

Advertisements

6 thoughts on “Maombi Juu ya Watoto

 1. Nashukuru sana, nami nitaomba maana ni kweli watoto wetu wanakutana na mambo mengi. Wanamuhitaji Mungu sana.

 2. Madawa ya kulevya ni tatizo kubwa ambalo watoto wetu wanakumbana nalo. tumuombe sana Mungu awaepushe.

 3. Kubakwa na kulawitiwa kwa watoto ni wimbi kubwa kwa Taifa letu tuombe Mungu awalinde watoto wetu jamani ni Mungu pekee anayeweza kuwaepusha.

 4. Hakika hatuwezi kuwalinda watoto wetu dhidi ya vita ya ibilisi katika ulimwengu wa sasa, isipokuwa kwa njia ya MAOMBI. MUNGU anawapenda watoto wetu na amethibitisha hilo kwa njia ya YESU. Mungu anasema watoto wetu watalindwa na hawataonewa. Isaya 54:13-14

 5. amen ni kweli wapendwa kuna umuhimu wa kuomba kwa bidii kwa ajili ya watoto wetu.Maana katika hali hii ya utandawazi changamoto ni nyingi mno.
  isaya 54:13 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

  isaya 62 :6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako; ee yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku nyinyi wenye kumkumbusha Bwana msiwe na kimya wala msimwache akae kimya mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya kuwa sifa duniani.
  Hizo ni ahadi tayari tunazo kazi ni kumkumbusha Mungu wetu kwa kuwa yeye ni mwaminifu na hasemi uwongo.

 6. ni wazo zuri wapendwa kuweweka watoto wote mikononi mwa Mungu watu tunapoanza mwaka mpya 2016 Mungu awe nao na damu ya Yesu iwafunike popote watakapokuwa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s