Mzazi Mlee Mtoto Vyema

Ni muhimu sana kumuomba Mungu kwa ajili ya watoto wetu. Lakini hii haiondi jukumu letu katika kuwalea na kuhakikisha wanakuwa na maisha bora na salama. Mambo mengine yanawatokea watoto sababu ya uzembe wa wazazi. Inashangaza sana kumuona mzazi anampa ice cream mtoto wa miaka miwili kushuka chini. Ukimuuliza anasema anapenda, jamani mtoto anawezaje kupenda kitu asichokijua? Kama hujawahi kumpa atakipendaje? Je kila anacholilia unampa?

Lingine mtoto anafanya anachotaka mzazi yeye anafuata tu. Akitaka katuni sawa, kucheza tuu muda wote sana, akizira sawa, akilialia ovyo sawa…yani mtoto ndiye anapanga ratiba yake na ya mzazi. Hapa unamfanya mtoto kuona kuwa dunia ni kama yeye anavyotaka iwe na hakuna changamoto. Unamharibu sana sana na matokeo yako hutaweza kumsaidia akishakuwa.

Advertisements

3 thoughts on “Mzazi Mlee Mtoto Vyema

  1. shalom! tena hiyo inachangia sana kuharibu watoto hata watu wengine hawaheshimiwi kwasababu hiyo mtoto anajiona yeye ndo kila kitu,huwa inachukiza sana siku hizi watoto wadogo hawana heshima kabisa sababu malezi mabovu ya wazazi,wazazi tujitahidi kuwalea watoto katika maadili mema si kila kitu asemacho mtoto kipo sawa.

  2. Its veeery true hmm Kuna nyumba nlienda yaani mtt ni zaidi ya mtu mzima yani hadi mimi mgeni naona aibu mara kashika hiki mara like mara katukana mara katukana un tafrani na wazazi wana smile tu…….ni hatari

  3. Ni kweli, wazazi tujitahidi kuwalea wototo wetu vizuri. Malezi huanzia nyumbani so tujitahidi sana kufanya mambo sahihi majumbani kwetu maana watoto wanajifunza sana kutoka kwa wazazi na housegirls miaka hii. Pia wazazi tusidhani kuwaachia watoto uhuru kupitiliza ndo tunawajenga, big no tunawaanda kwenda kwenye dunia ambayo haipo. Mbarikiwe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s