Kama Mwana Mpotevu, Rudi Nyumbani

Mwanzoni ulikuwa ni mtu mwenye kumpenda Mungu sana. Ulikuwa mwenye bidii katika mambo yote ya Mungu, maombi, kujifunza neno, kushuhudia na ulijiweka mbali na dhambi. Haikuwa kazi kukataa mambo ambayo unajua hayampendezi Mungu. Kila mtu alijua jinsi unavyompenda Mungu na hawakuweza kuongea au kufanya yasiyofaa mbele yako.

Lakini sasa upo mbali sana na Mungu. Mwenyewe unashangaa ni nini kimetokea, huna kabisa shauku na mambo ya mungu kama mwanzo. Unatamani sana urudie hali ya mwanzo lakini umeshindwa. Roho yako inahangaika lakini mwili haupo radhi kabisa. Mambo ambayo mwanzoni ulikuwa huwezi kuyafanya sababu ni machukizo mbele za Mungu siku hizi hata hujifikirii mara mbili kabla ya kuyafanya.

Mungu bado anakupenda. Anakuita kwa upendo urudi kwake. Tazama ni wapi ulianguka, ugeuke, ukatubu na uanze upya na Yesu. Mwanampotevu alipogundua kosa lake hakuona aibu, alirudi kwa baba yake na kuomba msamha. Rudi kwa Mungu wako, anza upya na Bwana. Bwana yupo mlangoni anakusubiri, macho yake amekaza kuangalia njia uliyotokea alikuw kuwa utarudi. Usione aibu, Rudi kwa baba yako.

Advertisements

One thought on “Kama Mwana Mpotevu, Rudi Nyumbani

  1. asante dada..machozi yamenitoka niliposoma huu ujumbe maana umenigusa sana. Nilikuwa active kwenye mambo ya Bwana lakini siku hizi nimepungua sana hadi rohoni mwangu najua. Mungu baba ninaomba unisadie tena kwa upya.

    Chris

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s