Uaminifu Katika Ndoa

Uaminifu katika ndoa ni jambo la kila mmoja, sio la mke peke yake. Inashangaza sana kuona watu wakisema kuwa mwanaume hawezi kukaa bila kutoka nje sababu ndivyo walivyo. Kweli?? Hivi biblia kuna mahali inasema kuwa mwanaume ni kiumbe dhaifu? Nini tofauti kati ya mwanadamu na mnyama kama mwanadamu unasema ulishindwa kujizuia eti ni shetani. Yaani unakuta mwanaume katembea nje ya ndoa tena mara nyingine hadi kupata  mtoto akiulizwa anajitetea mara ni shetani, mara nilipitiwa mara mke wangu ndio kasababisha sababu ya hili na lile.

Halafu utakuta analazimisha mkewe amsamehe na haoni kwa nini ashindwe kumsamehe na kila mtu anamshangaa mkewe kwanini amsamehi wakati wanaume ndivyo walivyo na hata kumlaumu mke kuwa ndio sababu. Wakati mke akitoka nje ya ndoa hakuna anayetaka kusikia sababu yoyote tena hao wanawake wanaomlaumu mume akitoka nje ya ndoa ndio wanakuwa wa kwanza kumlaumu na kila mtu anamwambia mume muache huyu mwanamke hakufai. Hivi watu wanapoapa kuwa waaminifu mume huapa kuwa nitakuwa muaminifu kama mke akifanya hili na lile? Hivi wanaume hamuoni kuwa mnajidhalilisha kusema kuwa ulishidwa kujizuia? Ina maana hauna tofauti na jogoo anayemkimbiza kuku na kumaliza haja zake pale anaposikia hamu? Mtu utafute namba ya simu, muwasiliane, mkubaliane, utoke ulipo hadi gest upange foleni reception, upande ghorofani chumbani, uvue nguo bado tu unajitetea hukudhamiria, kweli? Huyo shetani alikufunga kamba?

Usidhani mkeo hapati vishawishi, tena inawezekana vikubwa kukushinda lakini aliahidi uaminifu kutoka moyoni sababu anakupenda na kumheshimu Mungu. Hakuna sababu yoyote inayoweza ku justify mwanandoa kwenda nje ya ndoa. Kila mmoja aheshimu viapo vya ndoa na kumuogopa Mungu. Hii ndiyo silaha pekee ya ndoa.

Advertisements

4 thoughts on “Uaminifu Katika Ndoa

  1. Asante sana mpendwa kwa kutukumbusha juu ya hili.
    Wengi leo hii tunapotoshwa na mazoea ambayo hayana msingi wa kiMungu.
    Huwa naambiwa na watu kuwa hakuna mwanaume mwaminifu, wote huwa na agenda za siri nyuma ya pazia. Daima huwa nalipinga hilo na namuomba Mungu abadili fikra zetu tusiishie nasi kupoteza uaminifu kwa kufuata wasemayo watu.
    Mungu awe nasi wanandoa wa leo hasa tulio wachanga katika uwanja huu.

  2. Bwana asifiwe wapendwa!Nimebarikiwa na masomo ya kwenye blog hii!Binafc napenda nichangie kidogo kwenye mada hii,ujuwe swala la ndoa ni pana sana na huwa wapendwa wengi tunatumia akili zetu ktk kuoana na mara nyingi tunapomwomba Mungu thn tunaona kama anachelewa kujibu!hapo utakuta tunaingia kwenye ndoa na watu ambao c chaguo letu.Pengine wengine wana Do kabla ya ndoa!Hivi unategemea nini!Then isue ya ndoa ambayo imetoka kwa Mungu lazima upewe unayefanana naye.Na unayefanana naye lazima akupende,akuridhishe kimapenzi n.k.Haya mambo ya kukurupuka au kuwa na haraka ndiyo tunajikuta tunapewa tucyofanana nao thn mziki ndiyo unapoanza mara hawezi kuvumili mara mambo kibao yacyokuwa na kichwa wala miguu.Kingine uvuguvugu unatucost hatucmami imara na Mungu wetu.Mungu wetu c muongo so ukicmama naye no majuto!Huyo m.ume anayetoka nje hana nguvu ya Mungu analeta usanii kwenye wokovu!Mimi kabla cjaokoka nilikuwa napenda sana warembo hata wyf wangu alipata tabu sana bt aftr kumpata Jesus kiu ya mademu ilikwisha kabisa…

  3. Naendelea..Kiu ya mademu ilikwisha kabisa na c kwa juhudi zangu bt nimewezeshwa na RM!So no biashara ya kutoka nje!Tatizo wapendwa tunaleta usanii kwenye wokovu!Na c swala la wanaume tu bt hata wakina mama ambao hajacma na Mungu wanatoka nje sana!Tena wanafuata mapenzi tu!Wengine utackia huyu mume wangu c chagua langu so naishi naye tu!Hata haniridhish kimapenzi!Kabla cjaokoka nilishatembea na w.ke wengi ambao walikuwa wameokoka bt walikuwa wasanii na wanachokifuata zaidi ni ufundi bt c kingine!So nachotaka kusema m.ume au m.ke aliyecmama na Mungu no kutoka nje no majuto coz alipata anayefanana naye 100%.Kwaleo naishia hapa Mungu awabariki wote.

  4. NDOA NIKITU NJEMA SANA NILAZIMA KIHESHIMIWE SANA NA WANANDOA WENYEWE NA PIA WAJUE MAANA YA NDOA NI NINI NA JUKUMU LA KILA MWANANDOA JATIKA FAMILIA YAO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s