Mwamini Mungu Kwa Unayopitia

Mwaka unakaribia kuisha. Inawezekana mipango yako na maombi yako uliyokuwa nayo January mwaka huu hayajatimia hata moja, tena yamekua kinyume kabisa. Umekata tamaa, unaona kama Mungu amekuacha na kukusahau. Kila siku unasikia shuhuda jinsi Mungu anavyowatendea wengine, wewe umebaki unaomba usinipite mwokozi unisikie kila siku. Umefika mahali unaona utafute short cut maana ni kama Mungu hakusikii vile… Leo napenda nikutie moyo, Usikate tamaa. Mungu hufanya kazi zake kwa jinsi ya ajabu sana. Yeye hutuwazia mema, na wakati mwingine huruhusu tupitie hali fulani ili aweze kujitwalia utukufu.

Mungu alimruhisu shetani kumjaribu ayubu kupitia mali na mwili wale ili apate kujitwalia utukufu. Mungu anakuwazia mema, na hakika siku yako ipo. Japo usiku utadumu sana, lakini asubuhi yaja na utaacha kulia maana Bwana atakufuta machozi. Mungu wetu anabaki kuwa Mungu, hata asipotenda sawa na tunavyomuomba. Mungu alikuwa na uwezo wa kumtoa petro gerezani siku ya kwanza ila alimuacha hadi siku moja kabla ya siku ya kunyongwa, ili ajitwalie utukufu. Muamini Mungu kuwa anaona unayoyapitia na hakika atakuja kukuokoa na kukufanikisha. Mungu alikuwa amemuandaa Ruth kuwa ndani ya ukoo wa Yesu, lakini haikutokea tu, bali kwanza alipitia magumu mengi, alifiwa na mumewe, aliteseka ugenini ila yote hayo ilikuwa ni ili kukutana na mume ambaye Mungu amemkusudia, Boaz.

Unapitia nini? Mimi sijui ila Mungu wako anahua na hakika anakuja jukusaidoa navkukuvusha. Usitafute njia ya mkato, simama kwa uaminifu kwenye jaribu lako hadi mwisho ndipo utauona ushindi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s