Je Unajenga au Unabomoa Nyumba Yako?

Rebeka alikuwa binti mchapakazi, mchangamfu na mwenye upendo. Hayo yanadhihirika pale alipomchangamkia mgeni kisimani, akampa maji ya kunywa na kunyweaha na ngamia wake. Ngamia wanakunywa maji mengi sana, kwa binti kunywesha ngamia 10 maji ya kuchota kisimani lazima awe kweli mchapakazi na mkarimu. Uchapakazi wake na ukarimu ukampatia mume aliyetoka kwa Bwana.

Rebeka aliendelea kumtumaini Mungu na hata alipochelewa kupata mtoto alimngoja Bwana na alipoona kama watoto wanapigana tumboni alimwendea nabii wa Mungu ili amweleze tatizo ni nini na ndipo alipoambiwa kuwa atazaa mapacha, mataifa mawili na mdogo atamtawala mkubwa. Matatizo yanaanzia hapa, rebeka hakumweleza mume wake, usiri ukaingia ndani ya ndoa na alipopata watoto akawa anampendelea zaidi mdogo maana alikumbuka unabii. Alipoona kama Mungu anachelewa kutomiza ahadi na unabii wake akaamua kutumia udanganyifu ili mwanae ampendaye achukue baraka za kaka yake.

Usiri, kupendelea na udanganyifu ulikuja kusambaratisha kabisa familia, watoto wakawa na chuki na wazazi hawakuwa na maelewano mazuri. Mungu atusaidie, wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa wenye upendo, ukarimu, uchapakazi na utii lakini wanapopata watoto, kazi nzuri, kusongwa na ndugu n.k hujikuta wanaacha misingi ya mwanzo na kusababisha ndoa zao kuwa za matatizo na hatimaye kuvunjika. Je, ni jambo gani linakutoa katika mpango wa Mungu kwenye ndoa yako?

MIT. 14:1
“Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s