Tunahitaji Neema ya Mungu Kila Wakati

Wiki iliyopita nimesoma kwa mara nyingine tena maisha ya Sara na rebeka, wazazi wa mwanzo wa taifa la Israeli. Nimejifunza jambo lingine, hakuna mkamilifu bali tunahitaji neema na rehema za Mungu kila siku. Maisha ya mwanamke amchaye Mungu yamezungukwa na majaribu mengi sana sana. Sarah alikuwa mwanamke mtiifu sana, alimtii na kumweshimu mume wake siku zote, lakini jaribu la kutopata mtoto lilipozidi alikosa imani akaamua kulazimisha mtoto kupatikana kwa njia ya mkato. Baadaye alishindwa kukabili matokeo ya maamuzi mabaya akamtesa na kisha kumfukuza mjakazi wake.

Sarah hakua malaika bali mwanadamu, na hivyo Mungu hakumfutia ahadi yake kwake kwa sababu ya kosa lake, bado Mungu aliuangalia uaminifu wa Sarah na kumbariki kwa mtoto katika uzee. Na jina lake linaendelea kutajwa hadi katika agano jipya kuwa ni mwanamke mwenye imani na utii kwa Mungu na mume wake.

Tunahitaji kusogea katika kiti cha rehema ili kupata neema na rehema ya kutusaidia wakati wa uhitaji. No one is perfect and we are not super women, we need His grace daily.

EBR. 4:16
“Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”

Advertisements

One thought on “Tunahitaji Neema ya Mungu Kila Wakati

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s