Anza Mwaka na Bwana

Salam za mwaka mpya
Unapokaribia kuanza mwaka mpya, anza na Bwana na kumbuka mambo yafuatayo:

1.Omba Mungu akujalie moyo mpya wenye kumpenda yeye zaidi.

EZE. 36:25-27
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.”

2. Sahau yaliyopita yaliyokuumiza moyo na uliyofanya vibaya na angalia yaliyo mbele yako.

FLP. 3:13-14
“Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”

3. Jifunze kutokana na makosa.

EBR. 12:10-11
“Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.”

4. Mngoje Bwana kwa saburi.

ZAB. 37:7
“Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.”
ISA. 40:31
“bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”

5.

Kumbuka

uaminifu wake ni

mkuu

sana.

OMB. 3:22-26
“Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.    Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.    BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.    BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.    Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.”

Nakutakia

baraka za Bwana kwa mwaka 2014. Bwana akupe kibali na

kutimiza

haja za moyo wako.

Advertisements

2 thoughts on “Anza Mwaka na Bwana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s