Panga Mipango ya Mwaka

Mungu ametupa nafasi ya kuwa na mwaka mwingine. Inawezekana mwaka jana ulipitia magumu mengi sana kiasi cha kukata tamaa kama utaweza kuja kufanikiwa tena. Ukiangalia mwaka mzima hauoni mafanikio ya aina yoyote, hivyo umeanza mwaka mpya ukiwa umekata tamaa na kuvunjika moyo.

Leo nakutia moyo, usikubali kupoteza tena mwaka mwingine kwa kuishi ukijihirumia na kujisikitikia. Amua kusimamia maisha yako huku ukimtanguliza Mungu. Tafuta muda wa kutosha, chukua daftari/ diary kisha andika mipango uliyokuwa nayo mwaka jana, nini kilienda vibaya na kisha tafakari unaweza kufanya nini tofauti ili kuweza kufanikiwa. Changanua kwa kina wapi ulikosea, wapi unahitaji kurekebisha, kama ni kujifunza zaidi, kuweka akiba, kutafuta mkopo, kuwa na discipline n.k. kisha andika mpiango unayotaka kuiendeleza na mipya ya mwaka huu na jinsi gani utaweza kuifikia.

Wengi wetu hufanya kosa la kuweka mipango bila kuchanganua kila siku utakuwa unafanya nini ili kuifikia mipango na malengo yako. Ni lazima uwe na mipango ya muda mrefu, muda wa kati na kila siku ili uweze kujua kama unafanya kazi kufikia ndoto zako ama la.

Nitakuja na somo ya jinsi ya kuweka mipango ya mwaka…

Advertisements

One thought on “Panga Mipango ya Mwaka

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s