Fanyia Kazi Ndoto Zako…

Usikubali mtu akukatishe tamaa kuwa huwezi kufanya jambo fulani. Kama umelifanyia utafiti ukaona linawezekana, umejipanga kulifanya na unaona kabisa ndilo unalotaka kulifanya, lifanye. Usisikilize watu wanaokukatisha tamaa. Wengi wetu huangalia yale ambayo hatuwezi kuyafanya, au tumetamani kuyafanya ila tunaogopa na kuwakatisha tamaa wale wanaojaribu kulifanya. Wanaokatisha tamaa hufanya hivyo kuogopa kuwa utafanikiwa na wao wameshindwa au wanaogopa kujaribu.

Miaka kadhaa iliyopita nilikiwa nataka kufanya jambo fulani na kweli nilijua kabisa nitafanikiwa, nilipoomba ushauri kwa niliowaona wanajua zaidi kuhusu mambo hayo walinikatisha tamaa sana kwa kwa sababu nilikuwa sijajiamimi nikaacha, ila niliumia sana moyo na hasa pale alipokuja kulifanya mwingine maana ilikuwa ni opportunity ya kufaa sana. Sasa nimejifunza na hakika naona ambavyo mtu unaweza kufika mbali sana kama utaweka nguvu zako zote kufanyia kazi ndoto zako na kutosikiliza wanaokatisha tamaa.

Fanya utafiti wa kutosha, Fanya kazi kwa bidii, Usikate tamaa na hakika kufanikiwa ni lazima. Mungu akiwa upande wetu hakuna aliye juu yetu.

Advertisements

2 thoughts on “Fanyia Kazi Ndoto Zako…

  1. Nashukuru sana kwa mafundisho na yamenifundisha na yamenibariki
    Mungu awape neema muendelee kutuelimisha mkituonya na kutuhabarisha!
    Joel
    0769107096

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s