Ndoa ni Zaidi ya Mapenzi

Mapenzi pekee hayatoshi kukufanya kuolewa au kumuoa mtu fulani. Unaweza kupendana na mtu, mkapendana kwa kasi yaani muda mfupi tu tangu mfahamiane mapenzi moto moto, kila dakika ni message, kila saa mnapigiana simu na kila wakati mnaonana. Unajiona yaani huwezi ishi bila yeye na unatamani mfunge ndoa hapohapo na kuanza kuishi pamoja. Wait…hapo sasa unahitaji speed gavana au wazungu wanasema reality check. Mapenzi ya msisimko kamwe sio kigezo cha kuwa na ndoa nzuri, sio kigezo cha kufunga ndoa maana hali hiyo ni ya msimu tu, siku mmeshaoana mnaishi pamoja na msisimko umeisha nini kitawaweka pamoja? Mmeokoka mnaona mnachelewa kujuana kiuhalisia hivyo ili msimkosee Mungu suluhisho mnaona ni ndoa, haya sasa mmeshaoana mmeshajuana weee na ule msisimko wa mwanzo umeisha, what next???

Ndio, lazima umpende mtu na mpendane ili muweze kuishi pamoja, lakini mambo haya ni ya muhimu kuzingatia kabla haujaamua kufunga ndoa. Je mtu huyo anaishi vipi na ndugu zake na watu wake wa karibu? Kadiri anavyoishi na ndugu zake ndivyo atakavyoishi na wewe baada ya msisimko kuisha. Je ni mtu aliyejaa malalamishi, ubinafsi, ubabe au mtu mnyeyekevu, mkarimu na mwenye kuwajali ndugu zake. Kama kwake kila ndugu yake na rafiki yake ni mbaya kasoro wewe, stop and think.

Je, anauhusiano gani na Mungu? Anauhusiano wake binafsi au tu kwa sababu wewe upo karibu na Mungu basi ili kukupata naye anajisogeza? Maisha yake ya binafsi yanamshuhudia vipi? Katika maongezi fahamu msimamo wake juu ya matumizi ya fedha, mahusiano na ndugu na pia mambo mbalimbali ya maisha. Halafu jiulize kama utaweza kuchukuliana naye na misimamo yake maana usijidanganye kuwa utambadilisha, ndoa ni kuchukuliana ila kila mmoja anamambo anayoweza kuyachukulia na asiyoweza.

Usifikiri tu kuwa sababu mnapendana basi mtafanana kwa kila kitu, hapana na ndoa inahitaji upendo, kuchukuliana, kujitoa, kusamehe, na kujali. Upendo usikufanye ukawa kipofu kwa mtu mwenye tabia ambazo hutaweza kuzichukulia kama ugomvi na kupiga, kukosa uaminifu, mdokozi, mbinafsi na mpenda makuu ambayo uwezo haupo.

Advertisements

5 thoughts on “Ndoa ni Zaidi ya Mapenzi

  1. Somo zuri kwa watarajiwa kabla hawajafanya maamuzi wazingatie haya,na sio kuangalia mambo machache tu,

  2. Mada nzuri na napenda nichangie kidogo!Ujuwe isue ya ndoa wapendwa 2cchukulie kama ni jambo la mchezo!na isue ya kumpata yule unayefanana naye inahitaji nidhamu ya hali ya juu!na isue ya kuoa 2kiipeleka kwa ku2mia ujuzi wetu eti nimchunguze,cjui ananipenda kweli,cjui hatabadilika nikwambie mpendwa hapo ni sawa nakusema ngoja nionje sumu 2one ina ladha gani!eti wengine wanachunguzana mpaka miaka5!mtaumia!kuna wa2 ni wasanii hata umchunguze miaka mingapi atakuwa smart kama unavyotaka wewe bt ukitaka ujute kubali kuoa au kuolewa naye uone moto wake!na isue ya ku2mia utalamu wako ni sawa sawa na kwenda kucheza kamali ya mchezo wa karata tatu!cjui unategemea utapata!2cdanganyane lazima 2fuate maandiko yanavyosema na kuyatii hapa no janja!mke mwema hutoka kwa BWANA tena anakupa unayefanana naye yaan ule ubavu wako halic aliyoutoa kumuumba yeye kwaajili yako!na mkionana kwa mara ya kwanza basi upendo ule utadumu mpaka cku mmoja atakapotangulia!huwa hauna limit ya speed govrnor!ukimpata yule wakwako ..naendelea

  3. naendelea… ukimpata yule wakwako yaani mambo yanakwenda automaticaly!atakujali,atakuthamini kama anavyojithamini yeye!atakuridhisha hata kitandani coz hata kama hamjaanza ku DO tayari hica zinakubali so akifanya juhudi kidogo tu yaani mnafika mlima kilimanjaro tena pale kileleni kirahic!cyo mambo yakuachwa chini mwenzako anafika kileleni peke yake!tena hata mkigombana hamhitaji mchungaji au mtu yeyote tena unakuta yanaisha automaticaly no kununa no kupinda mdomo!yaani ni full kufurahia ndoa!bt huwezi kumpata huyu pasipo kumtel God tena unapomtel uwe na imani,utii sheria za God,ucwe na haraka ya majibu coz YEYE huwa hawai wala hachelewi!eti wengine utackia nimeomba wee hata hatokei ninayempenda na umri unaenda mimi namkubali yeyote tu nitoe nuksi! hapo mpendwa unakimbilia moto tena moto kweli!wengine wanakuwa na wachumba zaidi ya mmoja tena ana DO nao wote thn anamwomba MUNGU!mpendwa tegemea maumivu tu!anyway ngoja kwaleo niishie hapa!MUNGU AWABARIKI WOTE.

  4. Ni kweli kabisa kila jambo lina linakanuni na taratibu za ili kufanyika kama inavyotakiwa .hivyo ni jambo la muhimu sana kufuata hizo kanuni na taratibu kama zilivvyokwa ili kutojilaumu baadaye katika maisha yako.Mungu alishaweka ivo vyote

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s