Acha Kujidharau Unaweza

Wengi wetu hatujiamini wala kuamini kama tunaweza kufanya jambo lolote la maendeleo, kubwa au hata kuwa na ndoto za kufanya hivyo. Inawezekana tangia mtoto umekuwa ukiambiwa kwamba huwezi, ukijaribu kitu unaambiwa acha utaharibu, darasani kila mtu anakuona huwezi hata ukinyoosha mkono kujibu swali mwalimu hakuangalii na akikuchagua unajikuta kwa hofu unajibu huku unatetemeka unaishia kuchekwa na darasa zima. Hali hiyo ikakufanya ukose kujiamini, hata ofisini huwezi kutoa hoja yoyote au changamoto, unakubali tu kila unachoambiwa.

Hata ukisema uwaze mambo makubwa nafsi yako inakucheka kuwa huwezi, huna uwezo huu wala ule. Hujiamini kabisa kama unaweza azisha kitu, kukisimamia na kukifanikisha.  Leo nataka ufanye jambo moja, kaa mahali peke yako, chukua notebook na kalamu kisha andika positive qualities ambazo unajua unazo. Usiangalie watu wanakusemaje, hapa ongea na moyo wako, jichunguze na andika zote ambazo unazo. Kisha baada ya hapo zitafakari, ziweke kwenye akili, moyo na nafsi yako na ujitamkie kwa kumaanisha. Ikiwezekana zibandike kwenye kioo chako ili kila unapokuwa unajiandaa kutoka unazisoma na kuzikumbuka. Fanya zoezi hili leo kesho nitakuja na muendelezo.

Advertisements

7 thoughts on “Acha Kujidharau Unaweza

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s