Unyanyasaji wa Kijinsia

Tatizo la ukatili wa kijinsia watu wengi huwa wanalikwepa kuliongelea hasa makanisani. Ukigusia unasikia mwanamke lazima awe mtii kwa mume wake na hakuna anayetaka kulijadili kwa undani. Ukatili wa kijinsia upo wa aina nyingi, kuna kunyimwa matumizi muhimu, kutawaliwa kwa mabavu, kudhalilishwa na pia kupigwa. Wanawake wengi wanaishi katika ndoa zilizojaa ukatili mwingi na akiomba msaada kanisani anaambiwa tu afunge na kuomba bila msaada mwingine.

Sikatai kuwa hakuna linaloshindikana kwa Mungu na wala hatuwezi kumuekea Mungu mipaka, ila je inapotokea mke kupigwa kila siku hadi watoto wanashuhudia, kipigo kikali hadi kushindwa kwenda kazini mama huyu afanye nini? Inafika hatua anatishiwa panga, au anapigwa na vyombo mbalimbali na wameishi kwenye ndoa muda mrefu huyu mama anatakiwa kufanya nini? Wengi wanashindwa kuripoti maana jamii itawasuta, wanaona watoto watateseka na kubwa zaidi wanawapenda waume zao. Jambo hili ni kubwa na linaumiza sana, leo tuliongelee kujua nini kifanyike.

Advertisements

2 thoughts on “Unyanyasaji wa Kijinsia

  1. Labda uwekwe mpango wa wanaume kupewa elimu zaid juu ya umuhimu na mchango mkubwa walionao wanawake katika jamii na ndani ya ndoa pia. Hii ni kwa sababu wanaume wengi bado wana fikra potofu juu ya wanawake.Labda hii itasaidia kwa wao kuwaheshimu wanawake maana wanaume wooote wametoka kwa mwanamke. JAMANI MWANAMKE NI MWANAMKE HATA AKIWA MCHANGA TAYARI NI MAMA YAKO HUYO MUHESHIMU

  2. Kwa mtazamo wangu naona kama ndugu, jamaa na marafiki wanavyokuwa busy kumfundisha mwanamke akijiandaa kuingia kwenye ndoa, ingekuwa hivyo hata kwa mwanamme kwani wengi awapati mafundisho kuhusu jinsi ya kuishi na mke. Barikiwa dada maana issue ya ndoa imekuwa gumu sana.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s