Wekeza Kwenye Ndoa Yako

Umeshaolewa… Umeshaoa… Japokuwa mtu uliyekuwa unampenda sana siye aliyekuoa, labda hakuonyesha interest au kuna mambo yaliwafanya msioane. Uliyempenda sana siye uliyemuoa, aliolewa na mtu mwingine, hakukupenda au kuna mambo yalisababisha msioane. Hiyo sasa ni past, funga huo ukurasa, mtoe kwenye mawazo na akili yako. Sasa ni wakati wa kuangalia ndoa yako, kujenga ndoa yako, kumpenda kwa dhati uliyeoana naye na kusonga mbele.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya upendo na msisimko wa upendo. Ndoa haijengwi na msisimko wa upendo (passion), bali hujengwa na upendo wa dhati kisha msisimko huiboresha. Upendo sio kisifa bali ni tendo. Amua kumtendea mema, kumpenda, kumfurahisha na kumuwazia mema mwenzi wako siku zote. Kila siku tafuta njia ya kumfurahisha, kumuinua na kumtendea mema siku zote.

Kuendelea kumfikiria mtu uliyempenda zamani ni kuwasha moto utakaoteketeza ndoa yako na maisha yako ya kiroho. Wekeza kwenye ndoa yako na utaona itakavyoimarika na kuwa ya kuvutia.

Advertisements

2 thoughts on “Wekeza Kwenye Ndoa Yako

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s