Mume Tambua Sifa za Mkeo

Mwanaume lazima utambue uzuri wa mke wako ili uweze kumuweka moyoni mwako kama muhuri. Wengi hubabaishwa na muonekano wa nje wa wasichana na wanawake wengine, hupumbazika na kuwaona wake zao hawavutii na sio wazuri. Anasahau kuwa alimchagua miongoni mwa wengi akamuoa kwa sababu alivutiwa naye na alitaka kuishi naye siku zote.

Sifa za mke sio sura, umbo, mavazi wala makeup, hivyo ni vya ziada, na huboresha sifa halisi na kamwe haviwezi kuwa mbadala. Sifa za mke zinaonekana pale anapoihudumia familia, anapokesha usiku kunyonyesha na kumhudumia mtoto mgojwa, anapokuwa mkarimu kwa watu wa nyumbani kwake, anapojaribu kuwa na amani na wakwe wanaomchukia na kumsema vibaya, anapokuvumilia katika uhaba wa mali na mahitaji, anapokuonyesha upendo hata pale ambapo haustahili, anapohakikisha maisha yake yote ameyatoa kwa Mungu na anaishi maisha ya imani.

Sifa hizi wanaume wengi huzifumbia macho, hawaoni thamani ya walivyonavyo hadi siku wakivikosa. Macho yapo kuangalia vya nje na kuona ni bora kuliko walivyonavyo, wanasahau kuwa hao wa nje wanawaona bora sababu hawana majukumu ya kuhangaika nayo kila siku kama mke uliye naye ndani.

Mume nakupa changamoto, ukitaka mkeo achanue, awe mwenye furaha daima na kuvutia siku zote hakikisha unathamini mchango wake katika maisha yako, thamini kila anachokofanya kwako, msifie, mpongeze, mtie moyo, Simama naye, uwe karibu naye kuliko mtu mwingine na utashangaa jinsi atakavyo stawi, na ku glow na kuwa kijana siku zote.

MIT. 31:10, 28-30
“Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.    Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,  Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.    Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.”

Advertisements

One thought on “Mume Tambua Sifa za Mkeo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s