Muweke Mwenzi Wako Moyoni Kama Muhuri!

Wanandoa wengi wanajikuta nje ya mstari sababu hawajawaweka wenzi wao ndani ya mioyo yao kama mihuri. Kwa sababu ya changamoto za maisha na watu wengi kutumia muda kazini zaidi kuliko nyumbani maana kila siku unaondoka alfajiri na kurudi usiku, watu wamejisahau na kujenga mahusino ya karibu na wafanyakazi wenzao kuliko mume au mke.

Wewe unajua umeoa au umeolewa, kwanini unajenga urafiki wa karibu na mtu wa jinsia nyingine hadi kufikia hatua ya kusaidiana kifedha bila mwenzi wako kujua, kila siku kwenda lunch pamoja na wakati mwingine kutoka out mwenzi akiwa safari kwa kisingizio cha urafiki, kushare emotions zenu na kuchart usiku na mchana?

Ukimuweka mwenzi wako ndani ya moyo wako kama muhuri kamwe huwezi kufanya mambo hayo. Tambua upendo una nguvu sana, kama kweli unampenda mwenzi wako utakuwa na ujasiri wa kusimamia ahadi yako na kulinda hisia zako. Intimacy ya aina yoyote ni kwa ajili ya mwenzi wako tuu, hata kama ni matatizo ya kazini, wa kushare naye ili kupata faraja ni mwenzi wako na sio mdada au mkaka wa kazini.

Kumbuka, wivu ni mkali kama jehanam!!! Usijeipata jehanam hapa duniani, maana mwako wake ni mkali kama mwako wa moto, heshimu ndoa yako.

WIM. 8:6
“Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s